array(0) { } Radio Maisha | Seneti imeahirisha kikao cha kujadili mfumo wa ugavi wa mapato
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Seneti imeahirisha kikao cha kujadili mfumo wa ugavi wa mapato

Seneti imeahirisha kikao cha kujadili mfumo wa ugavi wa mapato

Kikao cha Kamati Maalumu ya Seneti kilichonuia kujadili mfumo wa ugavi wa shilingi bilioni 315.5 kwa Serikali za Kaunti kimeahirishwa hadi kesho. Maseneta wameshindwa kuafikiana kuhusu njia mwafaka ya kusambaza mgao kwa kaunti huku wakiomba muda zaidi wa kujumuisha mapendekezo yao.

Kikao hicho kililenga kujadili jinsi kaunti zitatengewa fedha za maendeleo huku mfumo unaopendekezwa na wataalumu pamoja na Tume ya Ugavi wa Mapato CRA ukipingwa vikali na magavana.

Mfumo huo unaopendekeza migao kutolewa kulingana na idadi ya watu, umepingwa vikali hasa na magavana wa maeneo kame nchini wanaosema kuwa utazitenga kaunti zao hata zaidi.

Mfumo huo pia unapendekeza kaunti kupewa fedha kulingana na kodi inayokusanywa, miundo mbinu, hali ya umaskini miongoni mwa masuala mengine.

Maseneta wameahirisha kikao hicho kutoa muda zaidi kwa mapendekezo muhimu kujumuishwa huku tayari Baraza la Magavana likiteta kuwa mfumo huo utachangia kukwama kwa maendeleo kwani magavana walikuwa wametengea fedha miradi mbalimbali.

Mwenyekiti wa Baraza la Magavana, Wycliff Oparanya amesema kuwa magavana watapoteza kima cha Bilioni 18 iwapo mfumo wa sasa utatumika akiwataka maseneta kuhakikisha kuwa kaunti hizo zinafidiwa ili kufanikisha maendeleo.

Maseneta wamesema kuwa jukumu lao ni kulinda ugatuzi hivyo basi watahakikisha kuwa mfumo unaopendekezwa ni ule utazipa kaunti nyongeza ya mgao.