array(0) { } Radio Maisha | Kenya imerekodi vifo 12, idadi ya juu zaidi
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kenya imerekodi vifo 12, idadi ya juu zaidi

Kenya imerekodi vifo 12, idadi ya juu zaidi

Kenya leo hii imerekodi idadi ya juu zaidi ya watu waliofariki dunia kutokana na ugonjwa wa Covid 19 baada ya watu 12 kufariki dunia katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita na kufikisha idadi jumla ya vifo kuwa 197.

Wote waliofariki dunia wako jijini Nairobi ambapo watatu miongoni mwao wamefariki dunia wakiwa nyumbani. Waziri wa Afya Mutahi Kagwe ametangaza takwimu hizo akiwa jijini Nairobi.

Hayo yanahiri huku watu wengine 189 wakithibitishwa kuambukizwa virusi vya korona baada ya sampuli zao kupimwa katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita na kufikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa elfu kumi mia mbili tisini na nne. Watu 106 miongoni mwao ni wanaume huku wanawake wakiwa 83. Aidha umri wa walioambukizwa ni kati ya miaka 5 na 71. Kaunti ya Nairobi inaendelea kuongoza kwa idadi ya maambukuzi huku visa 147 vikirekodia, Kiambu 20, Machakos, 11, Kajiado 5, Mombasa 2.

Takwimu za waliopiwa katika kipindi cha saa 24 hata hivyo ni za chini huku Waziri Kagwe akisema hali hiyo imechangiwa na matatizo ya nguvu za umeme. Sampuli zilizopimwa katika kipindi hicho ni elfu moja mia mbili na tano.

Waziri Kagwe aidha amezungumzia kuambukizwa kwa wauguzi 22 katika Hospitali ya Pumwani jijini Nairobi akisema kwa sasa Wizara inatathimini hali hospitalini humo kubaini iwapo kuna haja ya kuifunga ama la.

Wakati uo huo, watu wengine 65 wamepona na kuruhusiwa kuondoka hospitalini hali inayofikisha idadi ya waliopona kuwa elfu mbili mia tisa arubaini na sita. 

Wizara ya Afya imewashauri watu wenye dalili za maambukizi ya virusi vya korona kuhakikisha wanapiga simu kwa nambari 719 ili washughulikiwe ifaavyo badala ya kurandaranda katika hospitali mbalimbali wakitafuta matibabu hali ambayo huenda ikachangia ongezeko la maambukizi ya virusi.

Waziri Kagwe aidha amesema serikali haitozi ada zozote inapowapima watu kwa halaiki ama inapowapima watu waliotangamana na walioambukizwa. Amesema shilingi elfu tano zinazodaiwa kutozwa na baadhi ya hospitali binafsi ili kuwapima watu ni za juu zaidi akisema hospitali za umma zinatosha shilingi elfu moja pekee kwa yeyote anayejiwasilisha mwenyewe kupimwa.

Wakati uo huo, Waziri Kagwe amewakosoa wale ambao wanasema hakuna korona akisema kwamba hali halisi kuhusu virusi hivyo inaendelea kudhihirika kila siku na kwamba  kila mtu anastahili kuwajibika ili kuepusha maambukizi zaidi.

Ili kupiga jeki juhudi za kuwafuatilia watu waliotangamana na walioambukizwa virusi vya korona, Wizara ya Afya imezindua magari ya thamani ya shilingi milioni 200 yatakayosambazwa kwenye kaunti 13. Kaunti zitakazonufaika na magari hayo ni Nairobi, Mombasa, Kiambu, Kajiado, Machakos, Nyeri, Migori, Busia, Uasin Gishu, Nakuru, Taita Taveta, Elgeyo Marakwet and Kisii.