×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Daktari wa kwanza kufariki kutokana na Covid-19 azikwa Bungoma

Daktari wa kwanza kufariki kutokana na Covid-19 azikwa Bungoma

Biwi la simanzi lilitanda katika kijiji cha Ndalu katika Kaunti ya Bungoma wakati wa mazishi ya daktari wa kwanza kufariki dunia kutokana na ugonjwa wa Covid-19, Daktari Doreen Adisa Lugaliki.

Familia yake imesema kuwa Lugaliki mwenye umri wa miaka 38 hakujua kwamba alikuwa na kisukari kabla ya kulazwa katika Hospitali ya Aga Khan Jumatatu iliyopita.

Lugaliki ambaye amemwacha mumewe na watoto wawili, ametajwa na familia yake kuwa mtu mwenye bidii ambaye alifanya kipau mbele maslahi ya wagonjwa wake.

Mazishi yake yamehudhuriwa na watu kumi na watano tu kulingana na mwongozo wa serikali wa kuzuia maambukizi ya virusi vya korona. Familia hiyo imetoa wito kwa Serikali Kuu kuweka mikakati ya kuwalinda wahudumu wa afya ambao wako mstari wa mbele wakati huu kuwahudumia wagonjwa wa Covi-19.

Aidha imesikitika kwamba haijapewa nafasi ya kumwaga mpendwa wao kwa njia inayostahili kutokana na maagizo ya kuzuia maambukizi ya virusi vya korona.

Mumewe Kituku Kinyae, amewashauri Wakenya kuendelea kujilinda ili kuzuia kuambukizwa virusi hivyo.

Chama cha Madaktari nchini KMPU,  awali kilitangaza kwamba marehemu aliambukizwa virusi vya korona na mwenzake kazini ambaye pia aliambukizwa na mgojwa.

Chama hicho,  kimemtaja marehemu kuwa shujaa aliyefariki dunia akiwahudumia wagonjwa huku kikitaka serikali kuanza kutekeleza mpango wa kuwapa wahudumu wa afya bima ya bila malipo wakati huu wa janga la korona.