array(0) { } Radio Maisha | Maeneo mengi ya kuabudia yatasalia kufungwa kuanzia kesho
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Maeneo mengi ya kuabudia yatasalia kufungwa kuanzia kesho

Maeneo mengi ya kuabudia yatasalia kufungwa kuanzia kesho

Maeneo mengi ya kuabudu yametangaza akuwa hayatarejelea shughuli za kawaifa kuanzia kesho licha ya serikali kutangaza kuruhusu maneneo ya hayo kufunguliwa.

Kanisa la Anglikana la All saints Cathedral limesema kwamba halitafungua kanisa hilo kwa siki kadhaa zijazo. Canon Sammy Wainaina wa kanisa hilo amesema hatua hii inalenga kuipa kamati maalum iliyobuniwa kuweka mikakati ili kudhibiti mamabukizi. Amewashauri waumini kufuatilia ibada kupitia mtandao na vyombo mbalimbali vya habati.

Kwingineko katika taarifa kwa waumini wake makanisa ya Christ is the Answer Ministries (Citam), ya Parklands Baptist, Nairobi Baptist Church na Jubilee Christian Church yamesema badala ayke yataendeleza ibada zake kupitia mitandao.

Kiongozi wa kanisa la CITAM anayeondojka Askofu  David Oginde amesema waumini hawataruhiwa kuhudhuria ibada makanisani, hadi maambukizi ya virusi vya korona yatakapopungua. Askofu wa Kanisa la Parklands Batist  Ambrose Nyangao amesema kuna idadi kubwa ya waumini ambao wanegpenda kuhudhuria ibada ila serikali imeruhusu watu mia moja pekee.

Askofu wa Jubilee Christian Church Allan Kiuna ametangaza kuwa ibada zitaendelea kupitia mitandao na mashirika mbalimbali ya vyombo vya habai.

Wakati uo huo, kamati ya Msikiti wa Jamia Mosque imetangaza kuwa msikiti huo hautafunguliwa kwa sasa.

Ikumbukwe katika mashrti mapya yaliyotangaza na serikali mapema wiki hii misikiti na makanisa yanaruhusiwa kurejelea ibada kuanzia kesho na kuhakikisha yanaweza mikakati kudhibiti maambukizi ya virusi vya korona.

Katika mashari hayo ya serikali,mafunzo ya Sunday School na Madrasa hayakuruhusiwa. Aidha watoto chini ya umri wa miaka kumi na mitatu na watu wa zaidi ya miaka hamsini na minane hawaruhisiwi kuingia katika maeneo hayo ya ibada.