array(0) { } Radio Maisha | Watu 278 zaidi wathibitishwa kuambukizwa korona; 3 wafariki dunia
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Watu 278 zaidi wathibitishwa kuambukizwa korona; 3 wafariki dunia

Watu 278 zaidi wathibitishwa kuambukizwa korona; 3 wafariki dunia

Watu mia mbili sabini na wanane zaidi wamethibitishwa kuambikizwa virusi vya korona nchini.

Katibu Mkuu wa Utawala wa Wizara ya Afya Daktari Mercy Mwangangi amesema takwimu hizo zimetokana na vipimo vya sampuli elfu moja mia nne na tatu zilizopimwa katika saa ishirini na nne zilizopita.

Idadi hii sasa inafikisha elfu tisa mia saba ishirini na sita, idadi jumla ya maambukizi nchini.

Wakati uo huo, watu tisini na tisa wamethibitishwa kupona na kufikisha idadi jumla kuwa elfu mbili mia nane thelathini na wawili.

Watu watatu zaidi wamefariki dunia na kufikisha jumla kuwa mia moja themanini na wanne.

Akizungumza kwenye Kaunti ya Kwale Daktari Mwangangi amezidi kuwahimiza wananchi kuzingatia masharti ambayo yamewekwa na serikali ili kudhibiti maambukizi zaidi.

Gavana wa Kwale Salim Mvurya amesema kaunti yake imeweka mikakati kuzuia watu wanaiingia nchini kutoka Tanzania kutokana na ukaribu wake na taifa hilo. Amesema wote wanaoingia lazima wapimwe kubaini iwapo wameambukizwa korona au la kabla ya kuruhusiwa kuingia nchini.