array(0) { } Radio Maisha | Kaunti ya Mombasa yasifiwa kwa kuweka mikakati ya kuzuia maambukizi
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kaunti ya Mombasa yasifiwa kwa kuweka mikakati ya kuzuia maambukizi

Kaunti ya Mombasa yasifiwa kwa kuweka mikakati ya kuzuia maambukizi

Serikali ya Kaunti ya Mombasa imetajwa kuwa mfano bora katika kuweka mikakati ya kukabili maambukizi ya  virusi vya korona mashinani.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema kuwa Kaunti hiyo inaongoza miongoni mwa kaunti zote 47 nchini katika utayarifu wa kukabili maambukizi. Kaunti hiyo kufikia sasa ina vitanda 432 vya wagonjwa wa Covid-19, vyumba kumi na viwili vya wagonjwa hao na vipumizi kumi.

Kagwe aidha ameiponmgeza Serikali ya Gavana Ali Hassan Joho kwa kuanzisha kituo cha kuwatibu watu wenye matatizo ya akili akisema hicho ni kituo cha kwanza nchini.

Waziri huyo amezihimiza kaunti nyingine kuhakikisha kuwa zimeweka mikakati ya kukabili virusi hivyo kupitia kuboresha vifaa vya matibabu.

Ikumbukwe kuwa Serikali Kuu imewataka magavana kuhakikisha kuwa kila kuanti ina vitanda angalau 300 na kuwaajiri wahudumu wa afya wa ziada 500.

Jana serikali ilisema kuwa haitaruhusu mgonjwa yeyote wa Covid-19 kusafirishwa jijini Nairobi kwa ajili ya matibabu ikisema kuwa wagonjwa wote watatibiwa kwenye kaunti zao ili kuzuia msongamano katika hospitali za Nairobi iwapo maambukizi yatazidi.