array(0) { } Radio Maisha | Kenya imerekodi visa 447 vya korona
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kenya imerekodi visa 447 vya korona

Kenya imerekodi visa 447 vya korona

Kenya leo hii imerekodi idadi ya juu zaidi ya maambukizi ya virusi vya korona kuwahi kuripotiwa nchini , siku chache tu baada ya serikali kutangaza kulegeza baadhi ya masharti ya kudhibiti maambukizi.

Katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita watu 447 wamethibitishwa kuambukizwa virusi hivyo baada ya sambuli  3,803 kupimwa na kufikisha idadi jumla ya maambukizi kuwa 8,975. Takriban sambali 200,311 zimepimwa humu nchini tangu kuripotiwa kwa kisa cha kwanza mwezi Machi.

Akizungumza katika Kaunti ya Mombasa wakati wa kutoa takwimu za maambukizi ya kila siku, Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema kuwa mtoto mchanga mwenye umri wa mwaka mmoja na mzee mwenye umri wa miaka 88 ni miongoni mwa wa 447 waliambukizwa.

Kagwe amewashauri watu wa jinsia ya kiume kuendelea kujilinda akisema kuwa wanaume wanaambukizwa zaidi virusi hivyo ikilinganishwa na jinsia ya kike. Miongoni mwa waliombukizwa 280 ni wa kiume huku huku 167 wakiwa wa kike.

Wakati uo huo, Kagwe amesema kuwa wagonjwa 64 wa Covid-19 wameruhusiwa kuondoka hospitalini baada ya kuthibitishwa kupona na kufikisha idadi jumla kuwa 2,657. Katika Kaunti ya Mombasa watu 738 wamepona korona huku wengine 335 wakiendelea kutibiwa nyumbani.

Hata hivyo,  watu wengine wanne wamethibitishwa kufariki dunia kutokana na Ugonjwa wa Covid-19 na kufikisha idadi jumla ya waliopona kuwa watu 173 huku serikali kwa mara nyingine ikiwataka Wakenye kuendelea kuzingatia zaidi maagizo yake ya kuzuia maambukizi.