array(0) { } Radio Maisha | Rais Kenyatta aondoa marufuku ya usafiri hadi kwenye kaunti za Nairobi, Mombasa na Mandera japo kwa masharti
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Rais Kenyatta aondoa marufuku ya usafiri hadi kwenye kaunti za Nairobi, Mombasa na Mandera japo kwa masharti

Rais Kenyatta aondoa marufuku ya usafiri hadi kwenye kaunti za Nairobi, Mombasa na Mandera japo kwa masharti

Marufuku ya usafiri ndani na nje ya kaunti za Nairobi, Mombasa na Mandera itakamilika kesho saa kumi alfajiri baada ya Rais Uhuru Kenyatta kutangaza kusitishwa kwa marufuku hayo. Katika hotuba kwa taifa, Rais Kenyatta hata hivyo amesema amri hiyo itatekelezwa kwa masharti ambapo serikali itatathimi hali kwa kipindi cha siku 21 na endapo maambukizi ya virusi vya korona yataendelea, marufuku nyingine itatolewa.

Licha ya uhuru huo wa usafiri, wahudumu wa magari ya umma watahitajika kuwa na cheti cha Wizara ya Afya vilevile sekta ya uchukuzi cha kuhakikisha wamezingatia sheria za kudhibiti maambukizi ya virusi vya korona kabla ya kuendelea na safari hadi kwenye kaunti ambazo awali zilikuwa na marufuku ya usafiri.

Rais Kenyatta hata hivyo amesema serikali haitakuwa ya kulaumiwa endapo watu wengi wataamua kusafiri kuelekea mashinani na kuchangia ongezeko la virusi vya korona. Amesema ni jukumu la kila mtu kuzuia maambukizi zaidi na kuilinda familia yake.

Wakati uo huo Rais Kenyatta ametangaza kufunguliwa kwa awamu kwa maeneo ya kuabudu. Ibada zitafanyika kwa muda usiozidi saa moja. Hata hivyo watoto hawataruhusiwa kuendelea na mpango wa Sunday school huku wale wa dini ya kiislamu wakiagizwa kutohudhuria madrasa. Watoto wenye chini ya umri wa miaka 13 na watu wenye umri wa zaidi ya miaka 58 na wale walio na matatizo mbalimbali ya kiafya  hawataruhusiwa kuhudhuria ibada.

Washikadau katika Sekta ya Elimu kwa upande wao wamepewa hadi kesho kuchapisha kalenda mpya ya masomo itakayozingatiwa. Safari za ndege za humu nchini zitarejelewa kuanzia tarehe 15 Julai hii huku zile za kimataifa zikirejelewa Agosti 1.

 

Hata hivyo marufuku ya kuwa nje kuanzia saa tatu usiku hadi saa kumi alfajiri itaendelea kutekelezwa kwa kipindi kingine cha siku thelathini. Marufuku ya kuandaa mikutano ya hadhara vilevile itadumishwa kwa siku nyingine 30 huku hafla mbalimbali mfano za harusi zikifanywa kwa kuzingatia masharti ya kutokuwa na idadi kubwa ya watu wanaohudhuria.

 

Rais Kenyatta ameelezea kusikitishwa na ongezeko la dhulma katika jamii kipindi hiki zikiwamo za kifamilia na dhulma dhidi ya watoto. Kutokana na hali hiyo, Rais Kenyatta amekiagiza kituo cha kukabili uhalifu kuvichunguza visa vyote vya dhulma na kuwasilisha ripoti kwa kipindi cha siku 30 zijazo ili wahusika wachukuliwe hatua.