array(0) { } Radio Maisha | Mbunge wa Lugari aachiliwa
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×
Mbunge wa Lugari aachiliwa

Mbunge wa Lugari Ayub Savula amehusisha kunaswa kwake mapema leo na siasa za ubabe wa ufuasi akisema kuwa analengwa kutokana na umaarufu wa mrengo wake.

Savula amepuuza madai ya kutozingatia taratibu za kudhibiti maambukizi ya virusi vya korona, akisema kukamatwa kwake kumechochewa kisiasa.

Akizungumza muda mfupi baada ya kuachiliwa, Savula amesema alikuwa amefika katika Kituo cha mafuta kujaza petroli katika gari lake kabla ya umati mkubwa wa watu kumtaka awahutubie. Savula amesema kuwa amenaswa wakati alipokuwa akihepa kuwahutubia wananchi kwani anafahamu vyema maagizo ya serikali ya kuzuia maambukizi.

Savula ambaye amezuiliwa kwa muda wa saa mbili katika Kituo cha Polisi cha Mumias, amesema kuwa amedhalilishwa huku wapinzani wao wakiruhusiwa kufanya mikutano bila kuhangaishwa na polisi.

Mbunge huyo ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Chama cha ANC amewasuta wanaomchafulia jina Rais Uhuru Kenyatta na kuhusisha jina lake na siasa za migawanyiko.

Polisi hivi maajuzi walitibua mkutano wa Kinara wa FordKenya Moses Wetangula na mwenzake wa ANC Musalia Mudavadi katika eneo Bunge la Malava huko Kakamega , huku mikutano  ambayo imekuwa ikifanywa na viongozi wanaohusishwa na Mrengo wa Rais Kenyatta ikiendeshwa pasi na tatizo, ukiwamo uliofanywa na Katibu Mkuu wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi COTU Francis Atwoli.


Polisi walifunga barabara ya kuelekea nyumbani kwa mbunge wa Malava Malulu Injendi ,ambapo shughuli hiyo ingefanyika na kuhudhuriwa na Naibu wa Rais William Ruto.

Aidha hafla mbalimbali za mazishi ya jamaa za watu wanaokosoa serikali imekuwa ikitatizwa na polisi ikilinganishwa na wale wa Kenyatta.