array(0) { } Radio Maisha | Viongozi wa Magharibi wajadili mustakabili wa siasa za eneo hilo
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Viongozi wa Magharibi wajadili mustakabili wa siasa za eneo hilo

Viongozi wa Magharibi wajadili mustakabili wa siasa za eneo hilo

Viongozi wa eneo la Magharibi kwa mara nyingine wamesema kuwa watahakikisha kuwa eneo hilo linatwaa uongozi wa taifa mwaka wa 2022.

Viongozi hao wamefanya mkutano katika eneo la Nambale kwenye Kaunti ya Busia kuangazia mustakabali wa siasa za Magharibi kuelekea uchaguzi wa mwaka wa 2022.

Wamesema kuwa watahakikisha kuwa viongozi wote wanaungano kufanikisha lengo hilo.

Viongozi hao wakiwamo Magavana, Maseneta na Wabunge kutoka vyama mbalimbali vikiwamo FordKenya, ANC na ODM wamesema kuwa hawatakubali kulazimishiwa kiongozi huku wakikashifu vikali kulengwa kwa viongozi wa eneo hilo na mifumo ya serikali.

Wamesema kwamba hatatatishwa katika azma yao ya kuinganisha jamii hiyo kwa ushirkiano na viongozi wenye maono sawa kabla ya uchaguzi ujao.

Wakiwalenga moja kwa moja Gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya na Waziri wa Ugatuzi Eugene Wamalwa wanaopinga kutimuliwa kwa magavana wanaotajwa katika sakata za ufisadi, wamesema kuwa viongozi wawili wanatumiwa kwa minajili ya kufanikisha malengo fulani huku wakazi wa Magharibi wakiendelea kutaabika.

Wamesema viongozi wanaojipea jukumu la kushinikiza kuwapo kwa umoja wa jamii ya Mulembe wanalenga