array(0) { } Radio Maisha | Maambukizi ya korona nchini Kenya yapita elfu saba
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Maambukizi ya korona nchini Kenya yapita elfu saba

Maambukizi ya korona nchini Kenya yapita elfu saba

Kenya sasa ina takriban watu elfu saba  mia moja themanini na wanane waliothibitishwa kuambukizwa. Idadi hii imeafikiwa baada ya watu wengine mia mbili arubaini na saba kuthibitishwa kuambukizwa katika saa ishirini na nne zilizopita.

Katibu Mkuu wa Utawala wa Wizara ya Afya Dakta Rashid Aman amesema mia mbili arubaini na saba hao ni miongoni mwa watu elfu nne mia moja, arubaini na saba waliopimwa, huku akisema mzee wa miaka mia moja ni miongoni mwa waliothibitishwa kuambukizwa.

Kwa mara nyingine,  Nairobi imeendeleaa kuongoza kwa idadi ya maambukizi ambapo leo  visa mia moja hamsini na  vitatu vimerekodiwa, ikifuatwa na Mombasa ambayo imerekodi visa thelathini na vitano, Kajiado ina visa kumi na vitano, Busia na Kiambu kumi na viwili. Kaunti za Uasin Gishu, Nakuru na Garissa zimerekodi zote visa vinne, kila kaunti huku Murang'a , Nakuru na Siaya zikirekodi visa viwili. Kaunti za Lamu na Nyamira zimerekodi kisa kimoja, kimoja.

Wakati uo huo, watu thelathini na tisa wamethibitishwa kupona na kuruhusiwa kuondoka hospitalini hivyo basi kufikisha idadi jumla ya waliopona nchini kuwa elfu mbili mia moja arubaini na nane. Hata hivyo, Watu wengine wawili wamefariki dunia na kufikisha idadi jumla kuwa hamsini na wanne.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Matibabu  Daktari patrick  Amoth ameeleza kwamba idadi ya watu wanaofariki dunia kutokana na COVID-19 ni ya chini kulinganishwa na mataifa mengine duniani, na kwamba kwa sasa Kenya i katika nafasi nzuri katika kukabili maambukizi ya virusi vya korona.