array(0) { } Radio Maisha | Wizara ya Afya yathibitisha takwimu za KEMRI kwamba watu milioni 2.6 nchini waliambukizwa korona bila kujua
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Wizara ya Afya yathibitisha takwimu za KEMRI kwamba watu milioni 2.6 nchini waliambukizwa korona bila kujua

Wizara ya Afya yathibitisha takwimu za KEMRI kwamba watu milioni 2.6 nchini waliambukizwa korona bila kujua

Huenda watu milioni 2.6 nchini waliambukizwa virusi vya korona, kisha wakapona bila kujua. Wizara ya afya imesema  ripoti hiyo ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa kwa ajili yake na Taasisi ya Utafiti wa Kimatibabu KEMRI na shirika la Welcome Trust.  Katibu Mkuu wa Utawala katika Wizara ya Afya Rashid Aman amesema idadi kubwa ya walioambukizwa ni wakazi wa Nairobi kwa asilimia 12, , wakifuatwa na wa Mombasa kwa asilimia 8.6.

Aman amesema utafiti huo ulifanywa kutumia damu iliyoko katika hifadhi ya kitaifa ya damu ili kubaini  jinsi virusi vya korona vimesambaa nchini na idadi kamili ya watu ambao huenda wameambukizwa.  

Taasisi hiyo imekuwa ikipima uwapo wa chembechembe za antibodies katika damu ya mtu ili kubaini wale ambao wamewahi kuambukizwa kisha kuvikabili virusi vya korona.

Aman hata hivyo, ameelezea kuwa ripoti hiyo si bainifu na haioneshi idadi kamili ya watu waliowahi kuambukizwa kwani sampuni zilizotumika ni chache mno, huku akielezea kuwa utafiti zaidi unaendelea.

Kauli hii pia imeelezewa na mtafiti wa KEMRI Daktari Edwine Baraza ambaye amesema kwamba damu iliyo katika hifadhi mara nyingi hutolewa na watu wenye umri mdogo hivyo haiwezi kuwakilisha idadi kamili ya Wakenya.

Kuhusu idadi kubwa ya walioambukizwa kutoonesha dalili zozote daktari Baraza amesema kuwa hali hii itasaidia hospitali nchini, kuwahudumia wanaolazwa.

Katika ripoti hiyo asilimia 12.4 ya sampuli za wakazi wa Nairobi zilikuwa na antibodies. Nairobi imefuatiwa na Mombasa ambapo ni asilimain 8.6 ya sampuli zilizopatikana nazo.

Maeneo mengine yenye viwango vya juu vya maambukizi ni eneo zima la Nyanza na eneo la kati, pia Uasin Gishu. Utafiti huo ulifanywa katika sehemu mbalimbali nchini kati ya Aprili tarehe 30 na Juni tarehe 16.