array(0) { } Radio Maisha | TIFA:Asilimia 37 ya Wakenya wamesema hawawezi kuhudhuria mazishi ya yeyote wakati huu wa janga la COVID-19
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

TIFA:Asilimia 37 ya Wakenya wamesema hawawezi kuhudhuria mazishi ya yeyote wakati huu wa janga la COVID-19

TIFA:Asilimia 37 ya Wakenya wamesema hawawezi kuhudhuria mazishi ya yeyote wakati huu wa janga la COVID-19

Asilimia 23 ya Wakenya wamesema hawawezi kumtembelea yeyote aliyekuwa na ugonjwa wa COVID-19 kisha akapona, huku asilimia 41 ya Wakenya wakisema kuwa hawawezi kuwaruhusu watoto wao wacheze na watoto wa yeyeote aliyeambukizwa virusi vya korona. Ni utafiti uliotolewa na Shirika la utafiti la TIFA.

Ripoti hiyo vilevile inaonyesha kuwa asilimia 37 ya Wakenya wamesema hawawezi kuhudhuria mazishi yoyote wakati huu hata kama idadi ya waombolezaji ni chini ya kumi na watano.

Hata hivyo, asilimia 79 wamesema wanaweza kwenda kupimwa kubaini iwapo wameambukizwa virusi hivyo , huku asilimia 8 wakisema kuwa wanamujua mtu mmoja ambaye ameambukizwa virusi hivyo.

Utafiti huo vilevile umeweka wazi ni kwanini idadi kubwa ya Wakenya wanahofia kupimwa, asilimia 23 wakisema wanahofia uchungu wakati vifaa hivyo vinaingizwa mdomoni na puani, asilimia 14 wakisema kuwa wanahofia kwenda karantini ya lazima huku asilimia 9 wakisema wanaohofia unyanyapaa.

Vilevile Virusi vya korona vimesabisha msongo wa mawazo asilimia 19 wakisema wanashindwa kupata usingizi,huku asilimia 21 wakisema hawana matumaini na kuwa na hasira kila wakati.

Siku ya Jumanne wiki hii TIFA ilitoa ripoti iliyonyesha kuwa asilimia 69 ya Wakenya wamepunguziwa mishahara tangu kuripotiwa kwa kisa cha kwanza cha maambukizi ya korona mwezi Machi mwaka huu.

Aidha, asilimia 43 wamesimamishwa kazi kufuatia Janga la korona  huku asilimi 22 wakikumbwa na makali ya njaa.