array(0) { } Radio Maisha | Mutyambai awataka wananchi kuzirekodi video za polisi wanaokiuka sheria na kumtumia
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mutyambai awataka wananchi kuzirekodi video za polisi wanaokiuka sheria na kumtumia

Mutyambai awataka wananchi kuzirekodi video za polisi wanaokiuka sheria na kumtumia

Inspekta Mkuu wa Polisi, Hillary Mutyambai leo hii amekabiliwa na maswali mazito kutoka kwa wananchi waliotaka majibu yake kuhusu masuala mbalimbali yanayoizonga Idara ya Polisi.  Miongoni mwa masuala hayo ni kukithiri kwa visa vya ufisadi katika idara hiyo, mauaji ya kiholela na kuitishwa hongo mara kwa mara na maafisa wa polisi. Mutyambai ameulizwa maswali hayo kupitia mtandao wa twitter kutumia alama ya reli #Engage the IG kwa kipindi cha saa moja kuanzia saa tano asubuhi.


Nikinukuu baadhi ya masuali yalioulizwa nikianza na
SAM MWAURA anasema
mbona sijatendewa haki kwa miezi tisa sasa baada ya kudhulumiwa na hata kuibiwa bidhaa zangu na afisa wa polisi anayehudumu katika eneo la Ruiru 

Mwingine kwa jina Amakanji Thomas anauliza, mbona maafisa wa polisi wasio valia sare rasmi wamekuwa wakiwakamata wakenya hata wenye maski katika eneo la Archives jijini Nairobi na kuwaitisha shilingi elfu moja

Akiwajibu baadhi ya waliomuuliza maswali, Mutyambai ametoa wito kwa Wakenya kunasa video za maafisa wa polisi wanaokiuka sheria wakati wa utendakazi wao na kuziwasilisha kwa Idara ya Polisi ili wachukuliwe hatua.
Mutyambai amesema baadhi ya visa vya polisi kukiuka sheria vimekuwa vikifanyika katika maeneo ya mashinani hali ambayo imekuwa ikitatiza hatua kuchukuliwa dhidi yao kwani ushahidi hukosekana.


Mutyambai aidha amesema Idara ya Polisi inaweka mipango ya kutoa mafunzo zaidi kwa polisi ili kukomesha visa vya ukiukaji wa sheria vinavyoendelezwa na baadhi yao. Lakini je, wananchi wako tayari kuzinasa video za polisi wanaokiuka sheria na kuziwasilisha kwa Inspekta Mkuu wa Polisi Hizi hapa hisia zao.

Ripoti iliyotolewa na Mamlaka ya Kuangazia Utendakazi wa Polisi, IPOA mnamo Juni 2 ilionesha kwamba watu 15 waliuliwa na maafisa wa polisi na wengine 31 kujeruhiwa kipindi hiki ambapo wamekuwa wakitekeleza maagizo mbalimbali ya kuzuia kusambaa kwa virusi vya korona.


Aidha IPOA inaendelea kuvichunguza visa 87 vilivyoripotiwa na wananchi kuhusu mauaji yanayodaiwa kutekelezwa na polisi, dhulma za kingono miongoni mwa dhulma nyingine.