array(0) { } Radio Maisha | Duale amshuruku Rais Kenyatta kwa kipindi alichohudumu katika wadhifa wa Kiongozi wa Wengi
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Duale amshuruku Rais Kenyatta kwa kipindi alichohudumu katika wadhifa wa Kiongozi wa Wengi

Duale amshuruku Rais Kenyatta kwa kipindi alichohudumu katika wadhifa wa Kiongozi wa Wengi

Mbunge wa Garissa Mjini, Adan Duale amemshukuru Kinara wa Chama cha Jubilee Rais Uhuru Kenyatta kwa kumwamini na kumkabidhi nafasi hiyo aliyoitumikia kwa muda wa miaka saba.

Katika taarifa yake baada ya kutimuliwa katika wadhifa huo na kukabidhiwa Mbunge wa Kipipiri Amos Kimunya, Duale aidha amemshukuru Naibu wa Rais William Ruto vilevile wanachama wa Chama cha Jubilee kwa kumsaidia kutekeleza majukumu yake wakati wa kipindi chake ambacho kimekamilika leo mchana.

Wakati uo huo amesema nyadhifa mbalimbali serikalini vilevile vyamani huwa na muda wa kuhudumu na wakati wa kuondoka ukifika, viongoz wanastahli kuondoka kwa tabasamu na kuwapisha wengine kuhudumu.

Amempongeza Kimunya kwa kuteuliwa kuchukua wadhifa huo vilevile wakazi wa Garissa waliomchagua na Wakenya kwa jumla, akiwashauri kuendelea kudumisha umoja na amani.

Aidha amesema anajivunia kuwa Kiongozi wa Wengi wa kwanza chini ya katiba mpya ya mwaka 2010 ambayo ilibuni serikali za kaunti.

Naibu wa Rais kwa upande wake amempongeza Duale kwa utendakazi wake katika muda aliohudumu katika wadhifa wa kiongozi wa wengine. Amesema Duale atasalia katika kumbukumbu ya uongozi wa taifa hili, historia itakapoandikwa.

Nikimnukuu kwa kiingereza:-

My brother Aden Duale, you are a great leader. For the last 8yrs, you discharged your responsibilities as our party's 1st Majority Leader with style, precision, passion and loyalty. My friend, when parliamentary history is written you will have a chapter. Mbele iko sawa na Mungu.

Seneta wa Elgeyo Marakwet, Kipchumba Murkomen ambaye alibanduliwa katika wadhifa sawa na wa Duale katika Seneti ameandika ujumbe huu nikinukuu kwa Kiingereza,


It’s a men’s club. Gender Equity achieved. Legacy secured. Congratulations Rais!  Mwisho wa nukuu.