array(0) { } Radio Maisha | Watu wengine 260 waambukizwa virusi vya korona nchini Kenya
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Watu wengine 260 waambukizwa virusi vya korona nchini Kenya

Watu wengine 260 waambukizwa virusi vya korona nchini Kenya

Kenya imerokodi visa mia mbili na sitini vya watu waliombukizwa Virusi vya Korona katika saa ishirini na nne zilizopita, na kufikisha idadi Jumla ya walioambukizwa nchini kuwa elfu nne, mia saba na thelathini na wanane.

Miongoni mwa walioambukizwa mia mbili hamsini na wanne ni Wakenya huku sita wakiwa raia ya mataifa ya kigeni.

Takwimu hizo zimetokana na kupimwa kwa sampuli elfu tatu, mia sita na hamsini na moja ambapo kufikia sasa, Kenya imepima jumla ya sampuli elfu mia moja na arubanini na kumi na mbili.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe ametangaza tawkimu hizo akielezea mikakati iliyowekwa na serikali kukabili Janga la Korona katika kipindi cha siku mia moja zilizopita tangu kisa cha kwanza kiliporipotiwa.

Hayo yamejiri huku kaunti za Nairobi na Mombasa zikiendelea kurekodi idadi kubwa ya maambukizi ambapo Nairobi pekee ina visa mia moja hamsini na saba, Mombasa arubaini na viwili, Kwale kumi na vitano, Kiambu kumi na vinne, Machakos tisa sawa na Kajiado 9 huku kaunti za Migori, Nakuru, Busia na Homabay zikirekodi visa vitatu vitatu.

Aidha kilifi ina visa viwili huku Kisii, Kisumu, Kakamega na Laikipia zikirekodi kisa kimoja kimoja. Wakati uo huo, watu ishirini na mmoja wamethibitishwa Kupona hivyo kufikisha idadi jumla ya waliopona Korona nchini kuwa elfu moja, mia sita na saba.

Hata hivyo, watu wawili wameaga dunia na kufikisha idadi jumla ya waliofariki kutokana na Korona kuwa mia moja na ishirini na watatu.