array(0) { } Radio Maisha | Wagonjwa 550 wa korona wahudumiwa nyumbani ili kupunguza msongamano hospitalini
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wagonjwa 550 wa korona wahudumiwa nyumbani ili kupunguza msongamano hospitalini

Wagonjwa 550 wa korona wahudumiwa nyumbani ili kupunguza msongamano hospitalini

Wagonjwa takriban 550 wa korona ambao hawana dalili za maambukizi, kwa sasa wanahudumiwa nyumbani baada ya serikali kuanza mpango wa kuwahudumia nyumbani. Waziri wa Afya, Mutahi Kagwe amesema mpango huo umekuwa na ufanisi mkubwa kwani hakuna aliyefariki dunia kwa kuhudumia nyumbani. Kufukia sasa wagonjwa 338 wameondolewa katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Kenyatta na wengine 212 katika Hospitali ya Coast General.

Aidha Mkurugenzi Mkuu katika Wizara ya Afya, Partrick Amoth amesema Wizara ya Afya imeweka utaratibu wa kuhakikisha wagonjwa ambao hali zao zitaana kudorora wakiwa nyumbani wanarejeshwa hospitalini.

Amesema mpango huo unatakelezwa kwa kuzingatia masharti ya Shirika la Afya Duniani, WHO ambapo miongoni mwa masharti hayo ni kuhakikisha wagonjwa wanaoruhusiwa kwenda nyumbani ni wale ambao hawana magonjwa mengine ambayo huenda yakahatarisha afya yao iwapo hawatahudumiwa hospitalini.

Kando na hayp Waziri Kagwe amewaonya wahudumu wa baa wanaoendelea kuhudumu licha ya kwamba serikali imepiga marufuku biashara hiyo kwa sasa akisema leseni zao zitatwaliwa na hazitarejeshwa.

Waziri vilevile amewaonya wanaofanya mikutano inayoshirikisha umma bila kuzingatia masharti ya kujikinga akisema tayari  serikali ilipiga marufuku mikutano ya umma na agizo hilo lingalipo.