array(0) { } Radio Maisha | Seneti kujadili suala la kumbandua ama kumsaza Waiguru siku ya Jumanne
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Seneti kujadili suala la kumbandua ama kumsaza Waiguru siku ya Jumanne

Seneti kujadili suala la kumbandua ama kumsaza Waiguru siku ya Jumanne

Wabunge na Wawakilishi wa Wadi kwenye Kaunti ya Kirinyaga sasa wanadai kwamba Kiranja wa Wengi wa Seneti Irungu Kang'ata anapanga njama ya kuusitisha mchakato wa kufanikisha kubanduliwa mamlakani kwa Gavana Ann Waiguru.

Wakiongozwa na Kiongozi wa Wengi wa Bunge la Kirinyaga Kamau Murango, viongozi hao wamedai kwamba hatua ya Kamati ya Shughuli za Seneti kupendekeza kamati ya wanachama kumi na mmoja kuzichunguza hoja zilizosababisha kubanduliwa kwa Waiguru ni njama ya Irungu Kang'ata kuhakikisha kwamba Waiguru anasalia mamlakani.

Hayo yanajiri huku wakazi wa eneo la Kutus kwenye kaunti hiyo wakiandamana leo hii wakiwataka maseneta wote kushirikishwa katika hatua ya kwanza ya kujadili hoja za kubanduliwa kwa Waiguru badala ya kamati maalum ya seneti.

Wakati uo huo akina mama kwenye kaunti hiyo wamejitokeza na kumtetea Gavana Waiguru wakisema ndiye Gavana wao na Bunge la Kirinyaga linapaswa kumpa nafasi ya kuwahudumia wakazi waliomchangua.

Ikumbukwe maseneta walio kwenye kamati maalum iliyobuniwa kuyachunguza madai yaliyosababisha kubanduliwa kwa Waiguru ni pamoja na Seneta Gideon Moi wa Baringo, Seneta Maalum Beth Mugo, Anuar Loitiptip wa Lamu, Mohamed Mahamud wa Mandera, Johson Sakaja wa Nairobi, vilevile seneta maalum Abshiro Halaqe.

Wengine ni Cleophas Malala wa Kakamega, Maseneta maalum Beatrice Kwamboka na Judith Pareno, Moses Kajwanga wa Homabay na Enock Wambua wa Kitui.