×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Maambukizi ya korona yafika 3,305 nchini Kenya baada ya watu wengine 90 kuambukizwa

Maambukizi ya korona yafika 3,305 nchini Kenya baada ya watu wengine 90 kuambukizwa

Idadi ya maambukizi ya virusi vya Korona nchini imeendelea kuongezeka, sawa na visa vya wanaopona huku wito ukitolewa kwa wananchi kutilia maanani maagizo yanayotolewa na Wizara ya Afya.

Kufikia leo, idadi ya maambukizi imefikia watu 3,305 baada ya visa vingine tisini vya maambukizi kuripotiwa kufuatia kupimwa kwa sampuli 2,419 katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita. Miongoni mwa walioambukizwa ni wanaume 62 na wanawake 28 huku wote wakiwa raia wa Kenya. Rishad Aman ni Katibu wa Utawala katika Wizara ya Afya.

Aidha, Aman ametangaza kufariki dunia kwa watu wanne na hivyo kufikisha 96, idadi ya waliofariki kutokana na ugonjwa wa Covid-19

Hata hivyo, habari njema ni kwamba idadi ya wanaopona na kuruhusiwa kwenda nyumbani vilevile imeonekana kuimarika kila uchao baada ya watu 72 kupona. Kwa jumla, Kenya imeripoti watu 1,164 waliopona kutokana na virusi vya korona.

Wakati uo huo, Aman amezindua rasmi Siku ya Kuchangisha Damu (World Blood Donar Day) ambayo itaadhimishwa Jumapili wiki hii huku akitoa wito kwa umma kujitokeza kuchangisha damu baada ya takwimu kubainisha kwamba shughuli ya uchangishaji wa damu imepungua kwa asilimia themanini.

Kwa mujibu Shirika la Afya Duniani, taifa lolote lile linahitaji asilimia moja ya painti ya damu sambamba na jumla ya idadi ya raia wake. Kwasasa, Kenya inahitaji kuwa na painti nusu milioni za damu kinyume na hali ilivyo ambapo serikali hukusanya chini ya painti 1,370 kila siku.