array(0) { } Radio Maisha | Margaret Kamar achaguliwa kuwa Naibu Spika wa Seneti bila kupingwa
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Margaret Kamar achaguliwa kuwa Naibu Spika wa Seneti bila kupingwa

Margaret Kamar achaguliwa kuwa Naibu Spika wa Seneti bila kupingwa

Seneta wa Uasin Gishu, Margaret Kamar ndiye Naibu Spika mpya wa Seneti baada ya kuapishwa rasmi leo hii kuchukua wadhifa huo uliowachwa wazi, baada ya kubanduliwa kwa Kithure Kindiki.

Kamar ameapishwa rasmi katika kikao cha alasiri cha Bunge la Seneti kilichoongozwa na Spika Kenneth Lusaka baada ya kukosa washindani katika wadhifa huo kufuatia kujiondoa kwao.

Baadhi ya maseneta wamemmiminia sifa tele Kamar wakimtaja kuwa kiongozi mchapa kazi wakielekezea imani kwamba atatekeleza jukumu lake kwa uadilifu. Miongoni mwa waliompongeza ni Kiongozi wa Wengi katika Seneti, Samuel Poghisio, mwenzake wa wachache James Orengo miongoni mwa wengine.

Aidha Kiranja wa Bunge Irungu Kang'ata ameutaja uteuzi wa Kamar kuwa utakaokuwa kielelezo hasa kwa watoto wa kike wenye maono ya kuwania nafasi za uongozi siku zijazo, kauli ambayo pia imeungwa mkono na baadhi ya maseneta wanawake waliozungumza.

Kamar alikuwa akipigiwa upatu na chama cha Jubilee kuwania wadhifa huo. Waliojindoa kwenye kinyanganyiro hicho ni Seneta Maalum Judith Pareno aliyekuwa akipigiwa upatu na Chama cha ODM, Charles Kibiru wa Kirinyaga, Stewart Madzayo wa Kilifi na Isaac Mwaura ambaye ni Seneta Maalum. Seneta Maalum Millicent Omanga ambaye awali alitangaza nia ya kuwania wadhifa huo, alijiondoa baada ya kukosa kuzirejesha karatasi za uteuzi.

Kindiki ambaye ni mwandani wa Naibu wa Rais, William Ruto aliondolewa katika wadhifa huo kwa madai ya kutokiheshimu Chama cha Jubilee na uongozi wake. Hata hivyo Kindiki alisema kuondolewa kwake kulichochewa kisiasa kwani alitekeleza jukumu lake kwa uadilifu