array(0) { } Radio Maisha | Aden Duale aponea shoka la Jubilee
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Aden Duale aponea shoka la Jubilee

Aden Duale aponea shoka la Jubilee

Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa Aden Duale ameponea shoka la Chama cha Jubilee wakati wa kikao cha wabunge kilichoongozwa na Rais Uhuru Kenyatta mapema leo hii.

Chama cha Jubilee kimefanya mabadiliko katika uongozi wake bungeni ambapo Kiranja wa Wengi Benjamini Washiali  na Naibu wake Cecily Mbarie wamevuliwa rasmi madaraka.

Rais Uhuru Kenyatta amemteua Mbunge wa Navakholo Emmanuel Wangwe kujaza nafasi ya Washiali huku Mbunge wa Igembe Kaskazini Maoka Maore akizaja nafasi ya Cecily Mbarire.

Aidha wakati wa kikao hicho Amos Kimunya ameteuliwa kuwa Katibu wa Muungano wa Wabunge wa Jubilee

Awali ilihofiwa kuwa Jubilee ingetangaza mabadiko zaidi katika uongozi wa kamati mbalimbali na kuwalenga Mbunge wa Kikuyu Kimani Ichunguzwa ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ,  David Pkosing wa uchukuzi, Julius Melly wa Elimu, Moses Kuria, Alice Wahome, Joseph Limo, na Glays Sholei.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Naibu wa Rais William Ruto, Katibu Mkuu Raphaeli Tuju na wabunge wote na kuondoa hofu ya awali kwamba huenda Ruto asingahudhuria.

Viongozi hao wametajwa waasi baada ya kutangaza wazi kuunga mkono azma ya Naibu wa Rais William Ruto kuwania urais mwaka wa 2022. Aidha wameshtumiwa kwa kudhalilisha uongozi wa Kenyatta na kupuuza mwongozo wa chama.

Spika wa Bunge la Kitaifa Justine Muturi anatarajiwa baadaye leo adhuhuri kutangaza rasmi mabadiliko hayo wakati bunge litakaporejelea vikao vyake.

Mabaliko hayo yamejiri huku Rais Uhuru Kenyatta akiweka bayana kwamba hatawavumilia viongozi wanaohujumu utendakazi wake.

Kenyatta alisema kwamba haoni tatizo kuwafurusha waasi muradi tu asalie na viongozi watakaunga mkono ajenda zake za maendeleo kwa taifa.

Ikumbukwe fagia fagia hiyo ilianzia katika Bunge la Seneti ambayo Kipchumba Murkomen, Susana Kihika na Kindiki Kithure walifurushwa.