array(0) { } Radio Maisha | Rais Kenyatta ataka kuharakishwa kwa mazungumzo ya kujadili utaratibu wa kurejelewa kwa shughuli za masomo
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Rais Kenyatta ataka kuharakishwa kwa mazungumzo ya kujadili utaratibu wa kurejelewa kwa shughuli za masomo

Rais Kenyatta ataka kuharakishwa kwa mazungumzo ya kujadili utaratibu wa kurejelewa kwa shughuli za masomo

Athari za janga la korona ni miongoni mwa masuala yaliyotawala hotuba ya Rais Uhuru Kenyatta wakati wa sherehe ya Madaraka huku akiiagiza Wizara ya Elimu kuharakisha mashauriano yanayoendelea kuhusu namna ya kurejelewa kwa shughuli za masomo katika shule na vyuo.

Rais Kenyatta amesema ni dhahiri kwamba janga la korona limekuwa lenye athari kuu kwa walimu, wanafunzi na wazazi, hivyo pana haja ya kutafutwa kwa suluhu ya haraka kuhusu kalenda yamasomo itakayozingatia baada ya shughuli za elimu kusambaratika nchini tangu kuripotiwa kwa kisa cha kwanza cha korona humu nchini  Machi 13 mwaka huu. 

Rais Kenyatta aidha ameiagiza  Wizara ya  Masuala ya Ndani ya nchi vilevile ya Afya kushauriana na viongozi wa kidini kuhusu utataribu mpya utakaotumika kuziendesha shughuli za kidini, huku masharti yaliyowekwa na serikali kuzuia maambukizi zaidi ya virusi yakifanywa kipaumbele.

Wiki iliyopita, Waziri wa Elimu, Profesa George Magoha alipokea ripoti kutoka kwa Kamati ya Elimu iliyopewa jukumu la kutathmini mapendekezo ya wakishadau mbalimbali wa elimu kuhusu namna ya kurejelea kwa shughuli za masomo nchini, miongoni mwa mapendekezo yakiwa kupiwa kwa wanafunzi wote na walimu kubaini iwapo wameambukizwa korona ama la kabla ya kurudi shuleni, vilevile kufanywa kwa mitihani ya kitaifa mwezi Aprili miongoni mwa mapendekezo mengine.

Aidha ili kuinusuru sekta ya utalii ambayo ni miongoni mwa zilizoathiriwa pakubwa na janga la korona huku wafanyakazi wakifutwa, Rais Kenyatta ameiagiza Wizara ya Fedha kuikabidhi sekta ya utalii na hoteli humu nchini shilingi bilioni 2 zitakazotumiwa kuwasaidia wafanyakazi katika sekta hiyo kujikimu kimaisha wakati huu mgumu.

Rais Kenyatta aidha ametangaza kuendelea kujitolea kwa serikali kuzisaidia kaunti kulikabili janga hili huku kufikia sasa ikiwa imetuma mabilioni ya fedha kwa kaunti. Si hayo tu, ametangaza mikakati mbalimbali ambayo serikali imeweka kufikia sasa kuwanusuru wananchi kutokana na ugumu wa maisha mfano kupunguza kodi inayotozwa bidhaa kutoka asilimia 16 hadi 14 ili kuepusha kupanda kwa bei ya bidhaa.

Rais aidha amesema maagizo zaidi kuhusiana na janga la korona yatatolewa hivi karibuni kwa umma. Kwa upande wake, Naibu wa Rais, William Ruto amemhakikishia Rais Kenyatta kwamba ataendelea kumuunga mkono katika juhudi za kukabili korona. Ruto  ameelezea imani kwamba kupitia uongozi wa Rais, taifa litapata mwelekeo ufaao katika kulikabili janga hili licha ya kwamba hali haitakuwa kawaida na ilivyokuwa awali.

Ruto amezungumzia namna janga hili limeathiri pakubwa shughuli za kawaida kukiwamo kufungwa kwa shule, makanisa, kuathibirika kwa biashara nakadhalika, akisema hali hii ni ya kipekee ambayo haijawahi kushuhudiwa nchini.