array(0) { } Radio Maisha | Viongozi kadhaa wateuliwa kuwa wawakilishi wa eneo la Magharibi
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Viongozi kadhaa wateuliwa kuwa wawakilishi wa eneo la Magharibi

Viongozi kadhaa wateuliwa kuwa wawakilishi wa eneo la Magharibi

Seneta Cleophas Malala, Mbunge wa Navakholo Emannuel Wangwe vilevile Mwakilishi wa Kike wa Busia Florence Mutua wameteuliwa kuwa wawakilishi wa viongozi wa eneo la Magharibi katika vikao mbalimbali vya kuafikia mabadiliko kwenye Bunge la Kitaifa lile la seneti.

Viongozi hao ambao wamefanya mkutano na Katibu Mkuu wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi Nchini , COTU Francis Atwoli, wamesema wawakilishi wao wanajukumu la kuhakikisha eneo la Magaharibi haliachwi nyuma katika mabadiliko hayo vilevile kwenye mchakato wa kuifanyia marekbisho katiba.

Akizungumza baada ya mkutano huo, Seneta Cleophas Malala amesema jukumu kubwa walilo nalo ni kuhakikisha kwamba wanawaongoza maseneta vilevile wabunge wenzao katika kuhakikisha kwamba eneo hilo haliachwi nyuma katika michakato ya kuimarisha uongozi wa taifa. Amesema jukumu lao si katika mchakato wa kuifanyia katiba marekebisho pekee bali hata katika kuhakikisha kuwa viwanda vya eneo hilo vinafufuliwa.

Aidha Mbunge wa Saboti Caleb Khamis amesema mkutano huo umejadili kuhusu msimamo wa eneo la Magharibi katika mabadiliko yanayoendelea kufanywa bungeni vilevile msimamo wao katika kufanikisha kura ya maamuzi. Amesema wameafikiana kushirikiana bila kujali misingi ya vyama.

Mkutano huo umehudhuriwa na magavana wa eneo hilo, Waziri wa Ugatuzi Eugyne Wamalwa wabunge na maseneta wote wa eneo hilo.

Aidha viongozi wa Chama cha ANC Musalia Mudavadi vilevile wa FORD Kenya Moses Wetangula wamekosa kuudhuria licha ya kupewa mwaliko.

Mudavadi badala yake leo hii amekutana na Kinara wa Chama cha Narck Martha Karua, aliyekuwa Mbunge wa Gatanga Peter Kenneth vilevile aliyekuwa Mkuu wa Watumishi wa Umma wakati wa utawala wa Rais Daniel Arap Moi Sally Kosgei.

Mudavadi amesema wamejadiliana kuhusu masuala ya siasa vilevile maendeleo ya kitaifa. Ikumbukwe wiki jana Mudavadi alifanya mkutana na Kinara wa Ford Kenya Moses Wetangula.