array(0) { } Radio Maisha | Serikali yasisitiza kutofunguliwa kwa shule sasa ikizingatia maambukizi ya korona hayajadhibitiwa
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Serikali yasisitiza kutofunguliwa kwa shule sasa ikizingatia maambukizi ya korona hayajadhibitiwa

Serikali yasisitiza kutofunguliwa kwa shule sasa ikizingatia maambukizi ya korona hayajadhibitiwa

Kwa mara nyingine serikali imeapa kuwa haitaharakisha kufungua shule, ikisema visa va maambukizi ya virusi vya korona nchini vimeendelea kuongezeka.

Akizungumza alipopokea ripoti ya  Kamati Maalum iliyobuniwa kuangazia athari za korona katika sekta ya elimu na mikakati ya kuwezesha kurejelewa kwa shughuli za masomo, Waziri Magoha amesema kwamba usalama na afya kwa wanafunzi kwa sasa ni muhimu.

Magoha amesema atafuata aushauri wa wataalam wa afya akisema ataisoma ripoti hiyo kisha kujadiliana na washikadau wegine kuhusu hatua zitakazochukuliwa.

Ikumbukwe awali serikali ilikuwa imetaja kuwa huenda shule zikafunguliwa Juni tarehe 4, ila kutokana na hali ilivyo sasa huenda hatua hiyo ikachukua muda hata zaidi. Magoha amefafanua kuwa lengo kuu la kamati hiyo ni kuishauri serikali kuhusu kalenda ya masomo na usalama wa wanafunzi wala si kushinikiza tarehe ya kufunguliwa.

Akizungumzia mvutano baina ya baadhi ya shule za binafsi na wazazi Magoha amewataka kufanya mazungumzo kutatua migogoro yoyote ambayo imeibuka. Amesema shule za binafsi zinachangia pakubwa katika sekta ya elimu, na iwapo zitafungwa kutokana na ukosefu wa pesa basi wanafunzi ndio watakaoumia kwani hakuna nafasi ya kutoka katika shule za umma.

Baadhi ya mapendekezo katika ripoti hiyo, ni mitihani ya kitaifa kuaahirishwa hadi mwezi Aprili mwaka ujao, na shule kufunguliwa Septemba badala ya Juni mwaka huu.

Pendekezo jingine ni masomo kuendeshwa kwa awau hasa kwa shule za kutwa yaani kundi moja la wanafunzi kufika shuleni kipindi cha asubuhi na wengine alasiri, kando na kuwafanyia vipimo wanafunzi wote na walimu.

Kutoka na mapendekezo hayo kuhusu namna ya kurejelea kwa shughuli za masomo shuleni,  Mchambuzi wa masuala ya elimu na maendeleo ya kijamii, Adhiwo Obondoh, anaunga mkono suala la kufanyika kwa masomo kwa awamu ikizigatia shule nyingi na vyuo zina idadi kubwa ya wanafunzi