array(0) { } Radio Maisha | Watu 140 walioambukizwa korona watafutwa baada ya kutoa taarifa za uongo kuwahusu
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Watu 140 walioambukizwa korona watafutwa baada ya kutoa taarifa za uongo kuwahusu

Watu 140 walioambukizwa korona watafutwa baada ya kutoa taarifa za uongo kuwahusu

Serikali inawatafuta watu mia moja arubaini waliobainika kuambukizwa virusi vya korona ila wakatoa taarifa za uongo kwa maafisa wa afya.

Akielezea kuhusu idadi kamili ya maambukizi humu nchini Kaimu Mkurugenzi wa Matibabu katika Wizara ya Afya Daktari Partrick Amoth amesema jumla ya wagonjwa mia sita sabini na mmoja wanaendelea akutibiwa katika hosptali mbalimbali.

Hayo yanajiri huku idadi ya maambukizi ya virusi vya korona yakiendelea kuongezeka nchini kila siku huku sasa jumla ya maambukizi yakiwa elfu moja mia saba arubaini na tano. Leo hii watu wengine mia moja ishirini na saba wamethibitishwa kuambukizwa baada ya sampuni elfu moja mia tatu themanini na tisa kupimwa.

Katibu Mkuu wa Utawala wa Wizara ya Afya, Daktari Mercy Mwangangi amesema, Nairobi inaendelea kuongoza kwa idadi ya mambukizi huku leo visa sabini na sita vikiripotia, ikifuatwa na Mombasa na visa kumi na tisa, Busia kumi na sita Uasin Gishu vinane, Kajiado visa vitano, Kiambu viwili na kimoja Isiolo.

Jijini Nairobi Mtaa Wa Kibra kwa mara nyingine umerekodi visa vingi ambavyo ni arubaini na tisa, Ruaraka ni kumi na Vitatu, Makadara na Westlands vinne, Langata viwili na  huku mitaa ya Embakasi Magharibi, Kasarani, Dagoreti Kaskazini vile vile Starehe ikiwa na kisa kimoja.

Wakati uo huo, watu kumi na saba wamethibitishwa kupona na kuruhusiwa kuondoka hospitalini, na kufikisha mia nne thelathini na nane idadi jumla ya waliopona nchini. Hata hivyo watu wengine wanne wamefariki dunia wote wakiwa jijini Mombasa huku Daktari Mwangangi akisema walikuwa wakiugua magonjwa mengine.

Aidha amesema kwa sasa Wakenya wengi wanajitokeza kupimwa katika shughuli ya kuwapima watu kwa halaiki inayoendelea akisema hatua hiyo itaisaidia pakubwa serikali katika mipango yake ya kukabili maambukizi zaidi. Aidha ameendelea kuwashauri wakenya kufuata masharti yaliyowekwa na serikali.