array(0) { } Radio Maisha | Rais Kenyatta kupokea ripoti ya kamati ya elimu ya kushughulikia janga la korona
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Rais Kenyatta kupokea ripoti ya kamati ya elimu ya kushughulikia janga la korona

Rais Kenyatta kupokea ripoti ya kamati ya elimu ya kushughulikia janga la korona

Rais Uhuru Kenyatta leo anatarajiwa kupokea ripoti rasmi ya Kamati ya Elimu ya Kushughulikia janga la korona iliyoteuliwa kungazia athari za korona katika sekta ya elimu na mikakati ya kuwezesha kurejelewa kwa shughuli za masomo.

Takriban watu elfu tatu wamewasilisha mapendekezo yao kwa Kamati hiyo ya wanachama tisa inayoongozwa na Daktari Sara Ruto na ambayo imekuwa ikijumuisha mapendekezo yake kwa muda tangu kubuniwa wiki chache tu baada ya shule kufungwa Machi 15.

Huenda shule zikasalia kufungwa hadi mwezi Septemba iwapo mapendekezo ya awali ya washikadau katika sekta ya Elimu yatapitishwa na kamati hiyo.

Waziri wa Elimu profesa Geroge Magoha, aliratibu Juni 4 kuwa siku ya kufunguliwa kwa shule ila sasa huenda akalazimika kuzidisha muda huo  kutokana na ongezeko la maambukizi  nchini na shinikizo kwamba Kamati ya Ruto imemshauri kuweka Septemba kuwa mwezi wa kurejelewa kwa masomo.

Baadhi ya mapendekezo ambayo yamewasilishwa kwa kamati hiyo ni kuhakikisha kuwa serikali inatenga fedha za kutosha kufadhili elimu wakati huu mgumu, kubadili kalenda ya elimu, mikakata ya kulinda afya ya wanafunzi na walimu wakati shule zitakapofunguliwa miongoni mwa mengineyo.

Ripoti hiyo itawasilishwa siku moja tu baada ya Chama cha Kitaifa cha Walimu KNUT, Muungano wa Wafanyakazi wa Vyuo Vikuu, Tume ya Kitaifa ya Haki za Binadamu, Chama cha Madaktari KMPDU na Wanafamasia kupendekeza kuwa shule zisalie kufungwa hadi Septemba na mitahini ya kitaifa kufanywa Machi mwaka ujao.

Vyama hivyo aidha vimeitaka kamati yenyewe kuhakikishwa kuwa maslahi ya wanafunzi na walimu ni kipau mbele .

Hata hivyo, uamuzi wa iwapo shule zitafunguliwa Juni au la unasalia mikononi kwa Rais Kenytatta ambaye atapokezwa ripoti hiyi na Waziri Magoha .

Haya yanajiri huku Shirika la Afya Duniani WHO ikionya mataifa dhidi ya kuharakisha kufungua shule likisema kuwa  huenda hali hiyo ikasababisha kuzuka kwa awamu ya pili ya mlipuko kwa korona.

Aidha imesema kuwa janga la Covid -19 litasalia kwa muda na kwamba mataifa yaweke mikakati ya kuwawezesha wananchi kukumbatia hulla ya kudumisha usafi kila wakati.