array(0) { } Radio Maisha | Kenya imerekodi visa 123 vya korona; 3 wameaga dunia
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Kenya imerekodi visa 123 vya korona; 3 wameaga dunia

Kenya imerekodi visa 123 vya korona; 3 wameaga dunia

Watu mia moja na ishirini na watatu wamethibitishwa kuambukizwa Virusi vya Korona, katika saa ishirini na nne zilizopita na kufikisha idadi jumla ya walioambukizwa kuwa elfu moja, mia nne na sabini na mmoja.

Akitoa takwimu za kila siku za maambukizi ya Korona nchini, Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema visa vya leo vimekuwa vingi zaidi kuwahi kuripotiwa kwa siku moja, kutokana na idadi kubwa ya sampuli zilizopimwa ambazo ni elfu tatu na sabini na saba katika saa ishirini na nne zilizopitwa.

Miongoni mwa maambukizi hayo, visa themanini na vitano vimerekodiwa hapa Nairobi, ishirini na vinne Mombasa huku Kiambu ikiwa na vinne.

Waziri Kagwe amesema maambukizi  miongoni mwa jamii yameendelea kuongezeka hata zaidi, huku Mtaa wa Mathare Jijini Nairobi ukiwa na visa thelathini na vitano na kumi na vinne vikiwa Kibra.

Aidha, mtoto wa mwaka mmoja ni miongoni mwa waliothibitishwa kuambukizwa.

Hata hivyo, wagonjwa watatu wamefariki dunia huku ikiarifiwa kwamba wawili walikuwa wakiugua ugonjwa wa kisukari na mwingine saratani.

Kufia sasa watu hasmini na watato wamefariki duni Kutokana na Korona nchini humu huku Kagwe akiwasihi Wakenya kutolegeza kamba ya kudhibiti maambukizi zaiid.

Wakati uo huo, Kagwe amekariri kauli ya Rais Uhuru Kenyatta, kwamba Wakenya wanafaa kuzingatia masharti ya serikali bila ya kutegemea shinikizo la maafisa wa polisi katika kuzuia maambukizi ili kurejelea shughuli za kawaida.