array(0) { } Radio Maisha | Watu wengine 62 wathibitishwa kuambukizwa korona nchini Kenya
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Watu wengine 62 wathibitishwa kuambukizwa korona nchini Kenya

Watu wengine 62 wathibitishwa kuambukizwa korona nchini Kenya

Kenya imerekodi visa vingine sitini na viwili vya maambukizi ya korona na kufikisha idadi ya maambukizi kuwa elfu moja mia tatu arubaini na nane.

Akitoa tangazo hilo, Katibu wa Utawala katika Wizara ya Afya, Rashid Aman amesema watu hao wamethibitishwa baada ya sampuli elfu mbili mia mbili tisini na tatu kupimwa kwa kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita.

Hamsini na tisa miongoni mwa walioambukizwa ni Wakenya, na watatu wakiwa raia wa kigeni, huku umri wa walioambukizwa ukiwa kati ya miaka sita na sitini na minne.

Visa ishirini na vitatu miongoni mwa vilivyothibitishwa viko Nairobi, Mombasa kumi na sita, Kwale vinane, Kiambu sita sawa na Kajiado huku Kitui ikiwa na visa vitatu

Aidha wagonjwa wengine watatu waliopona wameruhusiwa kuondoka hospitalini. Kwa mara nyingine Aman amelalamikia hali ya watu wanaopimwa korona kutoa taarifa za uongo, hali ambayo inatatiza juhudi za kuwafuatilia hasa wanaoshukiwa kuambukizwa.

Aidha amesisitiza kwamba hakuna ada zozote zitakazotozwa kwa wanaotibiwa hospitalini kutokana na korona hivyo kutoa wito kwa wananchi kutohofia kupimwa.

 
Licha ya awali Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Huduma za Matibabu, Partrick Amoth kutangaza kwamba huenda Kenya ingeanza kurekodi visa kati ya mia mbili na mia tatu vya maambukizi mapya kila siku, Amoth amesema cha muhimu ni kwa wananchi kuzingatia masharti ya kujikinga ili kuepusha kufikia hali hiyo.