array(0) { } Radio Maisha | Wandani wa Ruto waendelea kulimwa kupitia mabadiliko
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Wandani wa Ruto waendelea kulimwa kupitia mabadiliko

Wandani wa Ruto waendelea kulimwa kupitia mabadiliko

Mirindimo ya kisiasa inaendelea kushuhudiwa katika Chama cha Jubilee huku wandani ya Naibu wa Rais, William Ruto wakiendelea kukabiliwa, tukio la hivi punde likiwa kuwaondoa baadhi yao katika kamati mbalimbali za seneti. 

Kwa mujibu wa mabadiliko hayo yaliyotangazwa na Kiranja wa Seneti, Irungu Kang'ata,  Seneta wa Nandi, Samson Cherargei ambaye pia ni mwandani wa Ruto, amepokonywa wadhifa wa Mwenyekiti wa Kamati ya Haki na Sheria, ambapo kwa sasa atalazimika kuchukua nafasi ya Kangata katika Kamati ya Kinga ya Kisheria Bungeni, Powers and Privilages committee.
 
Aidha Mithika Linturi wa Meru ameondolewa katika kamati muhimu ya Uhasibu wa Umma na Uwekezaji, Public Accounts and Investment  na nafasi yake kuchukuliwa na Seneta Fatuma Dullo.
 
Seneta wa Bomet, Christopher Lang'at ameondolewa katika Kamati ya Shughuli za Bunge, House Business Committee na nafasi yake kuchukuliwa na Seneta wa Nairobi, Johnstone Sakaja. Lang'at aidha amendolewa katika Kamati ya Elimu na nafasi yake kuchukuliwa na Seneta Alice Milgo.

Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen, ameteuliwa kuwa mwanachama wa Kamati ya Ugatuzi siku chache tu baada ya kutimuliwa kutoka wadhifa wa Kiongozi wa Wengi katika seneti. Aidha maseneta wengine walioondolewa katika kamati kuu wametafutiwa nafasi katika kamati nyingine.  Tayari Spika wa Seneti Ken Lusaka amefahamishwa kuhusu mabadiliko hayo ambayo yatatekelezwa mara moja.

Tayari baadhi ya viongozi walioathiriwa na mabadilo hayo wametoa maoni kupitia mitandao ya kijamii huku Murkomen akisema yu tayari kulihudumia taifa  katika wadhifa wowote ule sasa na hata siku zijazo. Ameendelea kusema nikimnukuu kwa kiingereza,

What I abhor is to take up positions at the expense of colleagues who are being humiliated for no apparent reason.

Mabadaliko hayo yanajiri huku Spika wa Seneti, Ken Lusaka akichapisha rasmi katika Gazeti Rasmi la Serikali kubanduliwa kwa Kithure Kindiki katika wadhifa wa Naibu Spika wa Seneti. Katika tangazo kwa maseneta kupitia spika wa muda, Rose Nyamunga, maseneta wanaotaka kuteuliwa kuhudumu katika wadhifa huo wametakiwa kutuma maombi yao kupitia kwa karani wa bunge hilo. Uchaguzi kwa wanaolenga wadhifa huo utafanyika siku ya Jumanne wiki ijayo.

Inaarifiwa kwamba maseneta wa Jubilee wanaomuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta na wale wa muungano wa NASA wanajadili suala la kumteua mmoja wao kuwania wadhifa huo.

Siku ya Ijumaa wiki iliyopita,  Kindiki aliondolewa katika wadhifa wa Naibu Spika kufuatia hoja iliyowasilishwa bungeni na Kiranja wa Wengini Irungu Kang'ata.

Kindiki alilaumiwa kwa kukosa kuhudhuria mkutano wa maseneta uliofanywa na Rais Uhuru Kenyatta Mei 11 na ambao uliafikia uamuzi wa kuwabandua maseneta Kipchumba Murkomen na Susan Kihika katika uongozi wa Seneti. Maseneta sitini na mmoja walipinga kura hiyo huku hamsini na wanne wakiunga mkono na saba wakipinga. 

Wakati wa kubanduliwa kwake, Kindiki alijitetea akisisitiza kwamba licha ya juhudi zake chamani, alilengwa visivyo akisisitiza haja ya maslahi ya Wakenya kufanywa kipau mbele badala ya siasa wakati huu wa maambukizi ya korona.