array(0) { } Radio Maisha | Kenya yaadhimisha Siku ya Afrika Duniani
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Kenya yaadhimisha Siku ya Afrika Duniani

Kenya yaadhimisha Siku ya Afrika Duniani

Kenya leo hii imejiunga na mataifa mengine kuadhimisha Siku ya Afrika Duniani, ambayo huwa kila mwaka tarehe 25 mwezi Mei. Akitoa hotuba yake kuhusu maambukizi ya korona nchini Kenya, Katibu wa Utawala katika Wizara ya Afya, Mercy Mwangangi amesema Kenya sawa na mataifa mengine Afrika itaendelea kushiriki vita dhidi ya janga la korona ambalo limetatiza pakubwa maisha ya kawaida kote duniani.

Aidha wasanii nao wamechukua fursa ya maadhimisho haya kuchanga fedha za kupiga jeki vita dhidi ya korona. Hayo yanajiri huku viongozi wakishauriwa kuzingatia zaidi sheria zinazozingira hali ya afya ya Waafrika kwa kuboresha afya yao. Wito huu umetolewa na Amira Elfadil Mohamed ambaye ndiye Kamishna Mkuu wa Masuala ya Kijamii katika Tume ya Muungano wa Mataifa ya Afrika.

Katika ujumbe ambao umetumwa kwa vyombo vya habari na tume hiyo, Bi Mohamed amewapongeza viongozi wa Afrika akisema tangu kuanzishwa na tume hiyo, Afrika imejizatiti iwezavyo kukabili majanga ya kiafya yanayoikumba bara hili.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Malaria, Kifua Kikuu na magonjwa mengine yanayoweza kuambukizwa katika tume hiyo Dakat Benjamin Djoudalbaye,  vifo vinavyosababishwa na malaria vimepungua Afrika kwa asilimia 66 katika kipindi cha miaka 15, na kuwa vifo vinavyotokana na UKIMWI vikapungua kwa zaidi ya nusu ya idadi katika kipindi cha miaka 10.

Amesema ana imani kuwa viongozi wa Afrika wana uwezo wa kukabili majanga yoyote yatakayolikumba bara hili kwa kuweka sheria mwafaka za afya.

Aidha Mkuu wa Mawasiliano na Masuala ya Afrika katika Kampuni ya Google, Dorothy Ooko, amehimiza haja ya kulinda utamaduni na haja ya watu kuzuru makavazi mbalimbali kujifunza utamaduni wa Kiafrika.
Ooko aidha amewashauri wapenzi wa Kiswahili kutumia mara kwa mara jukwaa la Google Translate ili kuwezesha mtambo kuwa na kumbukumbu ya maneno mengi ya Kiswahili vilevile miundo yake ya sentensi, hivyo kuwafaa wanaotumia jukwaa hilo kwa tafsiri.

Miaka 57 iliyopita, mataifa 32 ya Afrika yalikutana jijini Addis Ababab Ethiopia , kuanzisha Umoja wa Afrika AU.  Hata hivyo kando na maadhimisho ya AU, siku hii vilevile huwa ya kujivunia, kusherehekea,na kukumbatia, tamaduni mbali mbali za Afrika, umoja na utangamano.