array(0) { } Radio Maisha | Watu wengine sabini na wawili wamethibitishwa kuambukizwa korona nchin
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Watu wengine sabini na wawili wamethibitishwa kuambukizwa korona nchin

Watu wengine sabini na wawili wamethibitishwa kuambukizwa korona nchin

Watu wengine sabini na wawili wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya Korona katika saa ishirini na nne zilizopita na kufikisha idadi jumla ya waliombukizwa nchini kuwa elfu moja, mia mbili na themanini na sita.

Maambukizi hayo yametotokana na vipimo vya sampuli elfu mbili, mia saba na kumi na moja katika saa ishirini na nne zilizopita.

Katibu wa Utawala wa Wizara ya Afya Dkt. Mercy Mwangangi, amesema miongoni mwa walioambukizwa, sabini na wawili ni Wakenya, Msomali mmoja na Mganda mmoja.

Aidha, arubaini na wanne ni wavulana huku ishirini na wanane wakiwa wa kike.

Hata hivyo, Maeneo ya Nairobi na Mombasa yanazidi kurekodi idadi kubwa ya maambukizi, hivyo kuwashauri wananchi kutolegeza kamba ya kudhibiti Korona.

Miongoni mwa maambukizi hayo, Kaunti ya Nairobi pekee imerekodi visa hamsini na viwili ambapo ishirini na kimoja vimeripotiwa katika eneo la Lang'ata, kumi na vitano vikiwa vya Dagoretti kaskazini, Dagoretti Kusini imekuwa na kisa kimoja, Kamukunji visa vinne,  Kibra vinne, Embakasi Mashariki viwili, Kasarani vitatu huku Makadara na Mathare kukiwa na kisa kimoja kimoja.

Kaunti ya Mombasa imerekodi visa kumi na kimoja, Kiambu ikiwa na saba, Isiolo na Turkana zikiwa na kisa kimoja kimoja.

Kwa sasa Turkana imekuwa kaunti ya hivi punde kurekodi kisa cha Korona na kufanya idadi ya kaunti zilizoathirika kuwa ishirini na tisa miongoni mwa arubaini na saba.

Wakati uo huo, watu tisa wamethibitishwa kupona na kuruhusiwa kwenda nyumbani huku idadi jumla ya waliopona ikiwa mia nne na wawili.

Mgonjwa mmoja amefariki dunia na kufikisha idadi ya walifariki kutokana na Korona kuwa hamsini na wawili

Kuhusu majaribio ya aina ishirini na moja za chanjo ya Korona Duniani, Dkt. Mwangangi amesema Kenya inaendelea kushirikiana na taasisi za utafiti chini ya maelekezo ya Shirika la Afya Duniani WHO, katika juhudi za kutafuta chanjo salama kwa binadamu.

Hata hivyo, Mwangangi amesema kufikia sasa hakuna majaribio yoyote yanayofanyiwa nchini humu, na kwamba Shirika la Utafiti wa Matatibabu KEMRI linawakagua wagonjwa waliopona Korona kuona iwapo chembechembe za damu zao zinaweza kutumika katika kufanikisha upatikanaji wa chanjo.

Kuhusu malalamishi ya madereva wa matrela ambao wamekuwa wakilalamikia kunyanyaswa katika maeneo ya mipaka ya Kenyan a mataifa jirani kama Uganda na Tanzania, Kaimu Mkurugenzi wa Matibabu katika Wizara ya Afya Dkt. Patrick Amoth amesema serikali za mataifa haya mawili zinafanya mazungumzo ili kutafuta suluhu ya kudumu.