array(0) { } Radio Maisha | Watu 25 waambukizwa korona na kufikisha 912 idadi jumla nchini
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Watu 25 waambukizwa korona na kufikisha 912 idadi jumla nchini

Watu 25 waambukizwa korona na kufikisha 912 idadi jumla nchini

Idadi ya maambukizi nchini imefikia watu mia tisa kumi na wawili baada ya watu wengine ishirini na watano kuthibitishwa kuambukizwa.

Wizara ya Afya imepima sampuli 1,139 katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita na kufikisha jumla ya watu 44,581 ambao wamepimwa tangu kutangazwa kwa kisa cha kwanza cha maradhi ya Covid-19 nchini.

Miongoni mwa walioambukizwa, ishirini na watatu ni raia wa Kenya huku wawili wakiwa wa Somalia. Aidha ishirini na watatu ni wa jinsia ya kiume huku wawili wakiwa wa kike.

Akizungumza wakati wa kutoa takwimu za kila siku ya maambikizi, Katibu Mkuu wa Utawala katika Wizara ya Afya Daktari Rashid Aman amesem waathiriwa ni wa umri wa kati ya miaka ishirini na miwili na hamsini.

Walioambukizwa sita ni wakazi wa Kajiado, Mombasa watano, Nairobi ,Kiambu na Kwale watatu watatu kila moja, Taita Taveta wawili, Garissa wawili na Meru mmoja.Kufikia sasa kuna takribani kaunti ishirini na tatu ambazo zimeathiriwa na korona , Kaunti za Garissa, Meru na Taita Taveta zikiwa za hivi punde.

Maambukizi ya korona katika Kaunti ya Mombasa yanahusisha wakazi wa Likoni na Nyali,  huku ya Nairobi yakiwa ya Kawangware, Githurai 44,  na Starehe.

Visa vya korona katika Kaunti za Kajiado, Kwale na Taita Taveta vinawahusisha madereva wa matrela.

Daktari Aman aidha amesema kuwa watu ishirini na wawili wamepona na kuruhusiwa kuondoka hospitalini baada ya kupona huku idadi jumla ya waliopona ikifikia watu 336. Kufikia sasa Kenya ina watu hamsini ambao wamefariki dunia kutokana na janga la korona.

Serikali kwa mara nyingine,  imewaonya Wakenya dhidi ya kupuuza maagizo yake ya kuzuia maambukizi, Amani akisema kuwa maagizo hayo hayalengi kuwakandamiza bali kulinda afya yao.