array(0) { } Radio Maisha | Madereva 53 warejeshwa kwao baada ya kupatikana wemeambukizwa korona
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Madereva 53 warejeshwa kwao baada ya kupatikana wemeambukizwa korona

Madereva 53 warejeshwa kwao baada ya kupatikana wemeambukizwa korona

Serikali Kuu imesema kwamba itaendelea kulinda mipaka yake ili kuzuia maambukizi zaidi ya virusi vya korona kusambaa humu nchini.

Tayari serikali inaendelea kudhibiti safari za watu kuingia na kutoka mipakani, kwa kuwazuia madereva hamsini na watatu na kuwarejesha nchini mwao baada ya kupatikana na Korona.

Miongoni mwao hamsini na mmoja ni raia wa Tanzania huku wawili wakiwa wa Burundi. Waathiriwa wamepatikana wameambukizwa kufuatia upimaji unaondelea kwenye mipakana ya Namanga na Isebania.

Katibu Mkuu wa Utawala katika Wizara ya Afya Daktari Rashid Aman,  amesema uamuzi huo umeafikiwa hasa baada ya Kenya kufunga mipaka yake na mataifa ya Tanzania na Somalia kwa kipindi cha siku thelathini ili kuzuia maambukizi nchini.

Daktari Aman amesema kuwa serikali imeweka uzito mkubwa kwenye mipakani yake kufuatia hofu ya maambukizi ya juu nchini Tanzania.

Amesema kuwa shughuli ya kuwapima madereva wa matrela imefanikishwa baada ya kuzinduliwa kwa matumizi ya maabara tamba mpakani Namanga.

Idadi kubwa ya maambukizi kwa majuma matatu imekuwa ikiwahusisha madereva wa matrela wengi wakiwa raia wa Tanzania.

Tanzania ambayo ilisitisha shughuli za kutangaza takwimu za maambukizi ya Korona kila siku, imesema haitafunga mipaka yake kwa kuwa hali hiyo itaathiri pakubwa uchumi wake huku Rais John Pombe Magufuli akiwahimiza wananchi kuendelea kuchapa kazi kama kaiwaida.