×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Sossion amsuta Magoha kwa kuwapuuza walimu katika kukabili korona

Sossion amsuta Magoha kwa kuwapuuza walimu katika kukabili korona

Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu KNUT Willison Sossion ameendeleza shutma dhidi ya Wizara ya Elimu kwa kuvitenga vyama vya walimu katika kamati ya kushughulikia athari za korona katika sekta ya elimu. Sossion amesema kuwa KNUT haitatoa mapendekezo yake kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Sara Ruto,

Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, Sossion amemsuta Waziri wa Elimu Profesa George Magoha kwa kuwapuuza wawakilishi wa walimu katika masuala yanayowahusu walimu.

Katibu huyo amesema kuwa KNUT kwa ushirikiano na mashirika ya kijamii na wanachama wa vyuo vya umma wameafikiana kujumuisha mapendekezo yao kuhusu jinsi ya kusuru sekta ya elimu kutokana na janga la korona.

Sossion amesema kuwa chama hicho hakitaunga mkono mapendekezo ya kamati ambayo imewatenga washikadau muhimu kama vile Baraza la Magavana. Amesema Magavana wanajukumu katika mchakato wa kurejelewa kwa shughuli za masoma kwa kuwa wanawaajiri wauguzi na walimu wa chekechea katika  idara ambazo zimejerelewa.

Katibu huyo aidha amesema kuwa KNUT itashirikiano na mashirika mengine kupigania haki za wanafunzi na walimu huku akionya kuhusu kuharakisha kufunguliwa kwa shule akisema kuwa watalaamu wa afya wamesema iwapo Kenya itafungua shule mwezi ujao huenda vifo vikafikia elfu thelathini baada ya mwezi mmoja.

Kamati ya Ruto iliyobuniwa kuangazia athari za janga la korona katika sekta ya elimu ina wanachama tisa Mwenyekiti wa Muungano wa Wakuu wa Shule za Upili KESSHA, Kahi Indimuli, mwenzake wa shule za msingi Nicholas Gathemia, mwakilishi wa muungano wa shule za binafsi Peter  Ndoro, mwakilishi wa wazazi kupitia chama cha wazazi Nicholas Maiyo, mwakilishi wa kanisa katoliki Augustine Muthigani, mwakilishi wa shule za kimataifa Jane Mwangi, mwakilishi wa makanisa Nelson Makanda, mwakilishi wa dini ya kiislamu Sheikh Munawar Khan na mwakilishi wa shule za mahitaji spesheli Peter Sitienei.

Kamati hiyo pia itawashirikisha Ruth Mugambi wa Taasisi ya Mitalaa KICD, Patrick Ochichi wa Baraza la Mitihani, Gabriel Mathenge wa Tume ya Huduma za Walimu, Paul Libet, Anne Gachoya na Dkt Loice Ombajo wa Wizara ya Afya.