×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kenya imefunga mpaka wake na Tanzania vile vile Somalia

Kenya imefunga mpaka wake na Tanzania vile vile Somalia

Kenya imeifunga mipaka yake na Tanzania vilevile Kenya na Somalia, kwa siku thelathini kuanzia saa sita usiku leo.

Rais Uhuru Kenyatta amesema kufuatia mazungumzo na kamati ya kitaifa ya kushughulikia janga la korona nchini inayoongozwa na Waziri wa Afya Mutahi Kagwe imeafikiwa kuwa ndio njia bora ya kuthibiti mamabukizi zaidi.

Amesema hatua hii inafuatia kuongezeka kwa idadi ya visa vya mamabukizi ya korona, vilivyoripotiwa miongoni mwa watu walioingia nchini kutoka mataifa hayo mawili katika kipindi cha wiki moja iliyopita huku akisema maeneo ya mipakani baina ya mataifa hayo mawili yametambuliwa kuwa hatari.

Yatakayoruhusiwa kuingia na kutoka kwenye mipaka hiyo ni magari ya kusafirisha mizigo pekee, huku kukiwapo na mpango wa kuwapima madereva kubaini iwapo wameambukizwa korona au la.

Madereva hao hawataruhusiwa kuingia nchini iwapo watapatikana na Korona.

Rais amewashtumu wale wasioamini athari za virusi hivyo.

Ikumbukwe Tanzania haijaweka mikakati ya kudhibiti maambukizi ya virusi hivyo huku visa nchini humo vikiripotiwa kuendelea kuongezeka, japo takwimu za Tanzania hazitatolewa hivi karibuni.

Mara ya mwisho kwa Tanzania Bara kutangaza takwimu mpya za korona ilikuwa wiki mbili zilizopita Aprili 29, huku Zanzibar ikitoa takwimu mpya kwa mara ya mwisho wiki moja iliyopita Mei 7.

Kufikia sasa, watu 509 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya corona nchini Tanzania, huku 183 wakipona na watu 21 kufariki dunia.

Jumatatu wiki hii tiafa la Zambia lilifunga mpaka wake na Tanzania baada ya mamabukizi ya korona kuongezeka kwenye eneo la Mpakani la Tunduma.

Nchini Somalia watu elfu moja mia mbili themanini na nne wamethibitishwa kuambukizw akorona na wengine hamsini na watatu wakifariki dunia. Waliopona ni mia moja thelathini na watano.