array(0) { } Radio Maisha | Mshukiwa wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda, Félicien Kabuga amekamatwa

Mshukiwa wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda, Félicien Kabuga amekamatwa

Mshukiwa wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda, Félicien Kabuga amekamatwa

Mshukiwa wa mauji ya kimbari nchini Rwanda Félicien Kabuga, amekamatwa.

Kabuga ambaye amekuwa mafichoni kwa zaidi ya miaka ishirini kwa kuhusishwa na kupanga mauaji dhidi ya jamii ta Tutsi mwaka 1994 amekamatwa jijini Paris Ufaransa.

Kabuga amekamatwa kufuatia oparehsni kali ya maafisa wa uhalifu nchini humo, waliosema amekuwa akitumia jina tofauti.

Mshukiwa atafikishwa katika mahakama ya Rufaa ya Paris Kisha kupelekwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu iliyoko Hague Uholanzi ili kufunguliwa mashtaka.

Kabuga mwenye umri wa miaka themamini na minne, anaaminika kupanga na kufadhili mauaji ya zadi ya watu elfu mia nane.

Marekani ilikuwa imeahidi kutoa zawazi ya Dola milioni 5 ambazo ni sawa na shilingi bilioni mia tano na thelathini na tano na elfu mia nne, kwa yeyote ambaye angefanikisha kupatiklana kwa Kabuga.