array(0) { } Radio Maisha | Serikali kutangaza mikakati zaidi ya kuzuia maambukizi nchini
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Serikali kutangaza mikakati zaidi ya kuzuia maambukizi nchini

Serikali kutangaza mikakati zaidi ya kuzuia maambukizi nchini

Mazungumzo zaidi yanaendelea ili kubaini njia mwafaka ya kushughulikia maambukizi ya virusi vya korona nchini vile vile mikakati iliyowekwa na serikali kudhibiti korona. Rais Uhuru Kenyatta kesho anatarajiwa kutoa taarifa kuhusu hatua zaidi zitakazochukuliwa.  Katibu Mkuu wa Utawala wa Wizara ya Aga Rashid Aman amesema makataa ya amri ya kutopatikana nje kuanzia saa moja jioni hadi ya kumi na moja asubuhi yanakamilika kesho, hivyo kuna haja ya serikali kutoa mwelekeo zaidi. .

Hayo yanajiri huku idadi ya watu waliofariki dunia humu nchini kutokana na maambukizi ya virusi vya korona imefikia watu arubaini na watano baada ya watu wengine watatu kuthibitishwa kufariki leo hii. Wizara ya Afya aidha imethibitisha kuwa watu ishirini na watatu wameambukizwa virusi hivyo na kufikisha idadi jumla ya maambukizi kuwa mia saba themanini na mmoja.

Aman amesema kuwa miongoni mwa waliaombukizwa kumi na mmoja ni wa Nairobi, watano Mombasa, Kajiado watatu, Kiambu na Kajiadio wawili wawili. Waliambukizwa watano ni wa kiume huku kumi na wanane wakiwa wa kike. Katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita, takriban sambuli 2,100 zimepimwa.

Amesema kuwa visa vya Nairobi vinahusisha wakazi wa Embakasi, sita Kamukunji , Lang'ata viwili na Starehe Kimoja. Visa vitano vya Mombasa ni vya Mvita huku kile cha Kiambu kikiwa cha Thika. Aidha visa wivili vya Wajir vinahuhisha wakazi wa Wajiri Kaskazini. Visa vya Kajiado ni vya madereva wawili wa matrela wa maeneo ya Namanga na Bisil.

Amewapongeza wakazi wa mitaa ya Eastleigh na Oldtown jijini Mombasa kwa kuendelea kuzingatia marufuku ya kutoka na kuingia katika mitaa hiyo ili kuzuia maambukizi. Waziri kwa mara nyingine ameonya dhidi ya kupuuza maagizo ya serikali ya kuzuia maambukizi ya virusi vya korona.