array(0) { } Radio Maisha | Watoto wako salama dhidi ya ugonjwa hatari unaohusishwa na korona-Serikali
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Watoto wako salama dhidi ya ugonjwa hatari unaohusishwa na korona-Serikali

Watoto wako salama dhidi ya ugonjwa hatari unaohusishwa na korona-Serikali

Wizara ya Afya imetoa hakikisho kwamba watoto humu nchini wako salama dhidi ya maambukizi ya ugonjwa hatari usiojulikana ambao umeripotiwa kwenye mataifa ya Bara Uropa hasa Marekani ukihusishwa na virusi vya korona.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dakta Rashid Aman amesema kufikia sasa hakuna mtoto yeyote aliyeambukizwa korona ambaye ameonyesha dalili za ugonjwa huo ikiwamo miguu na mikono kuvimba, macho kuwa mekundu, midomo kupasuka na kuwa na upele mwilini.

Aman amehusisha ugonjwa huo ina idadi kubwa ya maambukizi ya korona kwenye mataifa hayo na kutoa hakikisho kwamba kufikia sasa watoto wa Wakenya wako salama dhidi ya maradhi hayo.

Watoto watatu tayari wamefariki dunia Jijini Newyork huku wanasayansi wakiendelea kuutafiti ugonjwa huo wenye dalili sawa na maradhi ya Kawasaki.

Wazira ya Afya nchini Marekani inaendelea kuwachunguza watoto themanini na watano ambao wameonesha dalili za ugonjwa huo.

Visa sawa na hivyo vimeshuhudiwa nchini Uingereza na maswali mengi yanaendelea kuibuka ni kuhusu watoto kutoathirika na ugonjwa huo katika mataifa ya Bara Asia ambayo yameathirika na korona.