×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Chama cha Mashinani CCM kitaungana na Jubilee

Chama cha Mashinani CCM kitaungana na Jubilee

Kupitia mtandao wake wa twitter, Guleid amesema kuwa  makubaliano hayo yatawasilishwa kwa msajili wa vyama vya kisiasa hivi karibuni.

Amesema wakati huu mazungumzo yangali yanaendelea kuhusu muungano huo wakati wachanganuzi wa kisiasa wakisema ni wakati wa Ruto kujitosa tena katika ulingo wa kisiasa baada ya kubwagwa na marehumu Joyce Laboso wakati wa uchaguzi wa mwaka wa 2017.


Mkataba huo utafuatia ule wa Jubilee na KANU siku ya Jumatatu,  baada ya kufanyika mkutano wa mabadiliko katika uongozi wa seneti baina ya Kenyatta na maseneta wa Jubilee.

Kikao hicho kiliafikia uamuzi wa kuwafurusha maseneta Kipchumba Murkomena na Susana Kihika huku nafasi zao zikijazwa na Samwel Poghisio na Irungu Kang'ata.

Chama cha Jubilee kimewafurusha maseneta watano wateule ambao walisusia mkutano huo siku moja tu baada ya wawili hao kupingwa kutimuliwa kwa mahakamani wakisema sheria ilipuuzwa

Kunatetesi za Jubilee kuendelea kuwaadhibu wanaokiuka maagizo ya Rais huku wabunge Kimani Ichung’wa wa Kikuyu na Kiranja wa Wengi Bungeni Benjamin Washiali wakiwa wanaolengwa.