array(0) { } Radio Maisha | Serikali kushughulikia malalamishi ya wahudumu wa afya
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Serikali kushughulikia malalamishi ya wahudumu wa afya

Serikali kushughulikia malalamishi ya wahudumu wa afya

Serikali inaendelea na mazungumzo na wawakilishi mbalimbali wa wahudumu wa afya ili kuhakikisha kwamba maslahi yao yanatekelezwa kikamilifu.

Katibu Mkuu wa Utawala wa Wizara ya Afya Daktari Mercy Mwangangi amesema Wizara ya Afya inafanya kila iwezalo kuwakinga wahudumu wa afya ambao wako mustari wa mbele katika vita dhidi ya korona kwa kuwapa vifaa vya kujikinga na virusi hivyo.

Akizungumza kwenye kikao cha hamsini na saba na wanahabari kuhusu maambukizi ya korona nchini, Mwangangi aidha amesema wizara hiyo leo hii imekabidhiwa vifaa vya kujikinga na korona kutoka kwa wahisani mbalimbali. Amesema leo hii takribani vifaa elfu kumi na moja vimepokezwa wizara hiyo tayari kutumiwa na wahudumu hao.

Amesema ana imani kuwa kabla ya Jumatatu wiki ijayo serikali na wahudumu hao watakuwa wamepata mwafaka kuhusu jinsi matakwa yao yatakavyotekelezwa.

Kauli ya Wizara ya Afya imejiri saa chache tu baada ya wahudumu wa afya kuapa kuanza mgomo wao Jumatatu wiki ijayo iwapo serikali haitaingilia kati na kutatua mgogoro baina yao.

Muungano wa Kitaifa wa Wahudumu wa Afya Kenya Health Workers Union Society umesema serikali imeendelea kuwatelekeza kwa muda wakati huu wanapoendelea kuwahudumia waathiriwa wa virusi vya korona, ukisema wanachama wake wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa virusi hivyo hatari.

Mwenyekiti wa Muungano huo , Peterson Wachira amesema juhudi zao za kuhakikisha kuwa inatekeleza matakwa yao kupitia mazungumzo zimegonga mwamba na sasa watagoma kuanzia Jumatatu ijayo.

Ni kauli ambayo imesisitizwa na Muungano wa Maafisa wa Maabara ,ambao umesema kuwa maslahi yao hayajashughulikiwa licha ya mara kwa mara kuwasilisha malalamishi yao katika Wizara ya Afya.

Mwenyekiti wa Muungano huo Claudia Talusa,  amesema imewalazim kujinunulia vifaa vya kujinga na virusi vya korona kutokana na hofu ya kuambukizwa.

 

Ikumbukwe Wizara ya Afya mapema mwezi Februari , ilitangaza kuwa imeanza mpango wa kuwafunza maafisa mbalimbali wa afya kuhusu namna ya kuwashughulikia waathiriwa wa virusi vya korona vilevile kuwapa vifaa vya kujikinga.