array(0) { } Radio Maisha | Mwanafunzi afukiwa mchangani Liteini Kericho
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Mwanafunzi afukiwa mchangani Liteini Kericho

Mwanafunzi afukiwa mchangani Liteini Kericho

Biwi la simanzi limetenda katika Kijiji cha Kusemek mjini wa Liteini kwenye Kaunti ya Kericho , baada ya msichana mmoja wa kidato cha tatu kufariki dunia wakati wa mkasa wa maporomoko ya ardhi.

Merehemu ni miongoni mwa wasichana watano waliokuwa wakichimba mchanga wakati wa tukio hilo.

Shughuli za kuwatafuta waathriwa wawili wa janga hilo bado linaendelea baada ya wengine kuokolewa wakiwa na majeraha mabaya.

Waathiriwa walikuwa katika harakati za kuchimba mchanga kujikumu wakati huu wa makali ya maambukizi ya korona. Wakazi wanasema huenda ikiwa vigumu kuwapata wawili hao kutokana na mvua kubwa ambayo imekuwa ikinyesha  na kulowesha ardhi.

Haya yanajiri huku Idadi ya watu waliofarikidi dunia kutokana na athari za mafuriko nchini,ikifikia mia mbili thelathini na saba, huku Wakenya elfu mia nane na kumi na saba wakiachwa bila makao baada ya makazi yao kusombwa. 

Waziri wa Ugatuzi Eugene Wamalwa amesema kaunti zilizoathirika zaidi ni Tana River, Garissa, Mandera na Kisumu.