array(0) { } Radio Maisha | Serikali imetenga KNUT katika kamati za kushughulikia athari za korona-Sossion
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Serikali imetenga KNUT katika kamati za kushughulikia athari za korona-Sossion

Vyama vya Walimu nchini vimeendeleza shutma dhidi ya Wazira ya Elimu kwa madai ya kuvitengwa katika mipango ya kuangazia mustakabali wa elimu nchini kufuatia janga la korona. Viongozi wa vyama hivyo wamemsuta Waziri wa Elimu Profesa George Magoha kwa kuwatenga kwenye kamati zinazojadili jinsi elimu itakavyorejelewa.

Katibu Mkuu wa Chama cha Kitaifa cha Walimu KNUT Willison Sossion, mapema leo amewasilisha malalamishi ya chama hicho kwa Magoha akilalamikia kutengwa kwa viongozi wa walimu kwenye kamati za kuangazia athari za janga la korona katika sekta ya elimu na ile ya kuweka mikakati ya kurejelewa kwa shughuli za masomo

Kupitia barua hiyo, Sossion amesikitishwa kwamba serikali imekiuka mwongozo wa sheria za leba ambapo walimu wanastahili kuhusishwa na wananchi kupewa nafazi ya kutoa maoni yao.Sossion amesema kuwa ni hatari kuwahusisha wasiokuwa wataalamu wa elimu kushughulikia salabasi.

Katibu huyo sasa anamtaka Waziri Magoha kuwahusisha walimu kwa kila hatua inayochukuliwa na serikali kuhusu mustakabali wa elimu nchini.

Awali Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu wa Shule za Upili na Vyuo vya Kadri, KUPPET, Akello Misori, alisema kuwa pana ya kujumuishwa muungano huo na ule wa KNUT katika kamati hiyo . Kadhalika amependekeza kujumuishwa kwa mwakilishi kutoka kwa Chama cha Madaktari na Muungano wa Wanafnzi wa Vyuo Vikuu vilevile wawakilishi wa vyuo vya kiufundi. Misori  amesema hatua itasaidia kufanywa kwa maamuzi ya haraka.

Kamati hiyo inaongozwa na Mwenyekiti Sara Ruto na inawanachama wanane wakiwamo Wenyeviti wa Walimu Wakuu wa shule za msingi na upili.

Wanachama wengine ni Mwenyekiti wa Muungano wa Wakuu wa Shule za Upili, KESSHA Kahi Indimuli, mwenzake wa shule za msingi Nicholas Gathemia, mwakilishi wa muungano wa shule za binafsi Peter  Ndoro, mwakilishi wa wazazi kupitia chama cha wazazi Nicholas Maiyo, mwakilishi wa kanisa katoliki Augustine Muthigani, mwakilishi wa shule za kimataifa Jane Mwangi, mwakilishi wa makanisa Nelson Makanda, mwakilishi wa dini ya kiislamu Sheikh Munawar Khan na mwakilishi wa shule za mahitaji spesheli Peter Sitienei.

Kamati hiyo pia itawashirikisha Ruth Mugambi wa Taasisi ya Mitalaa KICD, Patrick Ochichi wa Baraza la Mitihani, Gabriel Mathenge wa Tume ya Huduma za Walimu, Paul Libet, Anne Gachoya na Dkt Loice Ombajo wa Wizara ya Afya