×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Maeneo ya mipakani ni hatari kwa maambukizi ya korona Kenya -Wizara ya Afya

Maeneo ya mipakani ni hatari kwa maambukizi ya korona Kenya -Wizara ya Afya

Maeneo ya mipakani ndiyo hatari kwa maambukizi ya virusi vya korona humu nchini. Imesema Wizara ya Afya.

Katibu Mkuu wa Utawala wa Wizara ya Afya Daktari Mercy Mwangangi amesema maambukizi ya virusi hivyo yameongezeka kwenye maeneo ya mipakani, hasa ule wa Namanga na Isbania- Migori.

Mwangangi amesema mazungumzo yanaendelea na mataifa wanachama wa Muungano wa Afrika Mashariki kuhusu namna ya kukabili janga hilo.

Hayo yanajiri huku madereva wanane wa matrela Raia wa Tanzania wakirejeshwa kwao baada ya kupatikana kuwa wameambukziwa virusi vya korona. Wanane hao ni miongoni mwa watu elfu moja mia nne themanini na sita waliopimwa  katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopta.

Wakati uo huo, watu ishirini na mmoja wamethibitishwa kuambukizwa korona nchini, wanne wakiwa madereva wa matrela. Idadi jumla ya maambukizi ya korona nchini sasa imefikia watu mia saba hamsini na wanane.

Aidha watu watatu zaidi wamethibitishwa kupona na kufikisha idadi jumla kuwa mia mbili themanini na wanne. Hata hivyo idadi ya waliofariki dunia kutokana na korona sasa ni arubaini na wawili baada ya wengine wawili kufariki dunia jijini Nairobi.