array(0) { } Radio Maisha | Huenda virusi vya korona visikabiliwe -WHO
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Huenda virusi vya korona visikabiliwe -WHO

Huenda virusi vya korona visikabiliwe -WHO

Shirika la Afya Duniani WHO limesema kwamba huenda ikawa vigumu kuukabili Ugonjwa wa COVID-19 ambao sasa umewaathiri zaidi ya watu milioni nne kote duniani. Afisa wa WHO Mike Ryan amesema mataifa mbalimbali yanastahili kuweka mikakati kuhusu jinsi ya kukabili mamabukizi zaidi jinsi ambavyo virusi vya HIV vimeendelea kukabiliwa.

Ikumbukwe kufikia sasa kuna zaidi ya chanjo mia moja zinazoenelea kushughulikiwa na wanasayansi kwenye mataifa mbalimbali kuangamiza ugonjwa wa COVID-19.

Ryan amesema kuna magonjwa mengi yaliyo na chanjo ila hayajaangamizwa, kama vile ukambi akisema ni huenda ikachukua muda kwa suluhu ya kudumu kupatikana.