array(0) { } Radio Maisha | 4 wafariki dunia kutokana na korona 22 wameambukizwa
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

4 wafariki dunia kutokana na korona 22 wameambukizwa

4 wafariki dunia kutokana na korona 22 wameambukizwa

Kenya sasa ina jumla ya watu mia saba thelathini na moja  walioambukizwa virusi vya korona baada ya watu wengine ishirini na wawili kuthibitishwa kuambukizwa.

Katibu Mkuu wa Utawala wa Wizara ya Afya rashid Aman amesema watu elfu moja mia tano kumi na sita wamepimwa katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita.

Miongoni mwa ishirini na wawili hao ishirini na mmoja ni Wakenya huku mmoja akiwa raia wa Uganda.

Watu kumi ni wa jijiji Nairobi, wanane Mombasa, watatu Kajiado na mmoja ni wa Kaunti ya Bomet hivyo kufikisha ishirini jumla ya Kaunti ambazo zimeathirika.

Watu wanne zaidi wamefariki dunia kutokana na korona na kufikisha idadi jumla kuwa arubaini,  watatu wakiwa jijini Nairobi na mmoja Mombasa. Wakati uo huo, watu ishirini na wawili zaidi wameruhusiwa kuondoka hospitalini baada ya kuthibitishwa kupona. Jumla ya waliopona nchini ni watu mia mbili themanini na mmoja.

Aidha Aman amesema serikali ya Kenya imewapima madereva wa Matrela waliokuwa wakisafirisha mizigo mpakani pa Kenya na Tanzania kwenye eneo la Namanga ambapo ishirini na watano wamepatikana kuwa na virusi vya korona.Ishirini na watatu ni raia wa Tanzania, mmoja wa rwanda na mwingine wa Uganda na wote walikuwa upande wa Tanzania hivyo hawakuruhusiwa kuingia nchini.

Ili kuhakikisha kwamba maambukizi katika eneo la mipakani yanadhibitwa Aman amesema Kenya imepokea maabara tamba zitakazotumika kuwapina watu kwenye eneo la mipakani kubaini iwapo wana virusi au la.