array(0) { } Radio Maisha | Wakenya waliokuwa uchina kwa matibabu kurejea nchini leo
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Wakenya waliokuwa uchina kwa matibabu kurejea nchini leo

Wakenya waliokuwa uchina kwa matibabu kurejea nchini leo

Wakenya waliosafiri nchini India kwa matibabu maalum wanatarajiwa wakati wowote kuanzia sasa kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta.

Katibu wa Utawala Daktari Rashid Aman amesema Wakenya hao walikwama nchini humo baada ya serikali kusitisha safari zote za kimataifa za ndege kufuatia kuthibitishwa kuwapo kwa virusi vya korona nchini India.

Aman amesema kwa muda serikali serikali imekuwa ikijandaa kufanikisha kurejea kwao. Amesema Wizara ya Mashauri ya Nchi za Kigeni imekuwa ikiwasiliana na Serikali ya India kuhus jinsi ya kufanikisha kurejea kwa Wakenya hao.

 

Wakati uo huo Aman amesema Wakenya hao watalazimika kujiweka karantini kwa muda wa siku kumi na nne nyumbani kwao huku hali zao za kiafya zikiendelea kufuatiliwa na madakatri wao vilevile maafisa wa Wizara ya Afya waliojukumiwa kulikabili janga la korona.

Hapo jana Waziri wa Afya Mutahi Kagwe alisema wagonjwa hao hawatashurutishwa kukaa karantini kwenye ameneo yaliyotengwa na serikali ila watafuata ushauri wa madaktari wao.

Ikumbukwe wakenya hao sawa na walioko Uchina na Uingereza watagharamia safari zao hadi humu nchini. Kesho Ndege ya Shirika la Kenya Airways itaondoka nchini hadi jijini London, Uingereza kuwarejesha Wakenya waliothibitisha kuwa wako tayari kurudi.