array(0) { } Radio Maisha | Watu watano waliombukizwa korona wasakwa mombasa baada ya kutoroka
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Watu watano waliombukizwa korona wasakwa mombasa baada ya kutoroka

Watu watano waliombukizwa korona wasakwa mombasa baada ya kutoroka

Maafisa wa polisi kwa ushirikiano na wale wa afya kwenye Kaunti ya Mombasa wanaendelea kuwatafuta watu watano waliotoweka baada ya kubaini kuwa wameambukziwa virusi vya korona.

Watano hao ambao ni wakazi wa old Town Mombasa wanadaiwa kutoroka na familia zao muda mfupi baada ya kupata taarifa kwamba wana virusi hivyo.

Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho amesema kwamba washukiwa ni miongoni mwa watu sitini na watano waliopimwa juzi kupitia mpango wa kuwapima watu kwa halaiki mass testing ambao umekuwa ukiendelea.

Joho ameeleza wasiwasi kuwa huenda washukiwa wakasambaza virusi hivyo kwa watu wengine wengi zaidi jijini Mombasa .

Gavana huyo amesema watakapopatikana watadhibiwa kwa mujibu wa sheria.