array(0) { } Radio Maisha | Watu watatu wafariki dunia kutokana na korona na kufikisha 29 idadi jumla
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Watu watatu wafariki dunia kutokana na korona na kufikisha 29 idadi jumla

Watu watatu wafariki dunia kutokana na korona na kufikisha 29 idadi jumla

Idadi ya watu waliofariki dunia humu nchini kutokana na ugonjwa wa Covid -19 imefikia ishirini na tisa baada ya watu watatu kuthibitishwa kufariki leo hii. Haya yanajiri huku idadi ya maambukizi ikifikia watu 607.

Katibu Mkuu wa Utawala wa Wizara ya Afya Dakta Rashid Aman amesema kwamba waliofariki wawili ni wa Nairobi huku mmoja akiwa wa Mombasa. Aidha watu sabu wamepona na kuruhusiwa kuondoka hospitalini.

Akizungumza wakati wa kutoa takwimu za maambukizi nchini, Dakta Aman amethibitisha kuambukizwa kwa watu wengine ishirini na watano na kufikisha idadi jumla kuwa 607. Miongoni mwa walioambukizwa ishirini na wawili na raia wa Kenya na watatu wa mataifa ya Uganda, Tanzania na Uchina. Waathiri ni wa umri wa kati ya miaka minane na sabini.

Walioambukizwa kumi na saba ni wakazi wa Nairobi, wawili Wajir na Kajiado,  Mombasa, Migori na Nakuru kila mmoja mmoja. Visa vya Nairobi vimehusisha mitaa ya Eastleigh, Kawangware, Parklands, Riruta, South C na Juja Road. Kisa kimoja cha Mombasa na cha mtaa wa Likoni. Kufikia sasa  takribani kuanti 18 zimerekodi visa vya maambukizi nchini.

Aidha watu mia moja tisini na watano wanaendelea kutibiwa korona kwenye maeneo mbalimbali nchini huku mmoja aliyekuwa hali mahututi akiondolewa kwenye chumba hicho baada ya kupatana nafuu . Dakta Patrick Amoth ni Mkurugenzi Mkuu wa Matibabu katika Wizara ya Afya.