array(0) { } Radio Maisha | Wakazi wa Eastleigh na Oldtown waonywa dhidi ya kupuuza maruku ya kutoka na kuingia humo
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Wakazi wa Eastleigh na Oldtown waonywa dhidi ya kupuuza maruku ya kutoka na kuingia humo

Wakazi wa Eastleigh na Oldtown waonywa dhidi ya kupuuza maruku ya kutoka na kuingia humo

Wakazi wa mitaa ya Eastleigh Nairobi na old Town Mombasa wameonya vikali dhidi ya kupuuza marufuku ya kutotoka na kuingia kwenye mitaa hiyo.  

Katibu Mkuu wa Utawala katika Wizara ya Afya Dakta Rashid Aman amesikitika kwamba licha ya kuanza kutekelezwa kwa marufuku hayo wakazi wa Eastleigh wameonekana wakijaribu kutumia njia za mikato na kuingia kwenye mitaa jirani.

Rashid amesema iwapo Wakenya wataendelea kupuuza maagizo hayo basi huenda ikawa vigumu kudhibiti maambukizi ya korona kutokana na hali kwamba waathiriwa wengine hawaoneshi dalili za virusi hivyo. Amewahimiza Wakenya kuwaripoti wanaokwepa kutoka mitaa ya Eastleigh na Oldtown ili wakabiliwe kwa mujibu wa sheria.

Leo hii maafisa wa usalama wameimarisha doria mtaani humo kuhakikisha hakuna anayeingia wala kutoka. Kumekuwapo na vizuizi kumi na kimoja vya barabarani kwenye ameneo ya kuingilia na kutoka mtaani Eastleigh, hasa kwenye idadi kubwa ya watu.

Vizuizi viko kwenye eneo la Duka kuu Rikana na St Theresa Barabara hizi huunganisha mtaa wa Eastleigh na Shauri Moyo, Makongeni na Pangani .

Kulikuwa na kizuizi kwenue barabara ya Waruinge , Mzunguko wa  Kariokor r, Hospitali ya Kina mama kujifungua ya Pumwani Mna mzunguko wa Medina Mall.