array(0) { } Radio Maisha | Serikali imesema hakuna uwezekano wa masomo kurejelewa hivi karibuni
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Serikali imesema hakuna uwezekano wa masomo kurejelewa hivi karibuni

Serikali imesema hakuna uwezekano wa masomo kurejelewa hivi karibuni

Serikali Kuu imefutilia mbali uwezekano wa shughuli za masomo kurejelewa humu nchini hivi karibu ikisema kwamba shule zitafunguliwa iwapo tu maambukizi yatadhibitiwa kikamilifu.

Waziri wa Elimu Profesa George Magoha amesema kwamba afya ya wanafunzi ni kipaumbele wakati huu wa janga la korona na kuwa ni mapema mno kuanza kushinikiza ni lini masomo yatarajelewa.

Akizungumza mbele ya Kamati ya Elimu ya Bunge la Kitaifa alipotakiwa kueleza mustakabali wa elimu nchini, Waziri Magoha kwa mara nyingine amesema kwamba kalenda ya mitihani ya kitaifa itasalia ilivyokuwa.

Magoha aidha, amewahakikishia wazazi na wanafunzi kwamba walimu watapewa mwongozo wa jinsi ya kurejelea masomo kwa kuzingatia ni wapi mtalaa ulikomea kabla ya shule kufungwa.

Waziri Magoha vile vile, ameeleza mikakati zaidi ambayo imewekwa na serikali katika kufanikisha elimu ya wanafunzi kupitia mitandao wakati huu ambapo wako nyumbani. Miongoni mwa mikakati hiyo ni kuunganisha umeme mashinani kuwawezesha wanafunzi kufuatilia vipindi vya masomo kwenye radio na runinga na kuwapa mafunzo ya kidigitali walimu.

Waziri huyo amefika bungeni baada ya kususia vikao awali,  wabunge wakimkabili kwa maswali kuhusu mustakabili wa elimu nchini wakati huu mgumu.

Magoha aliyekuwa ameandamana na Katibu wa Elimu Belio Kipsang' amewatetea walimu wanaolipisha elimu ya mitandao ila amewaagiza kushirikiana na wazazi.

Kulingana na mwongozo uliotolewa awali na Wizara ya Elimu kuhusu kufunguliwa kwa shule mwezi ujao, likizo fupi ya muhula wa pili itafupishwa kwa siku nne, likizo ya Agosti ikifupishwa kwa majuma mawili na vipindi vya masomo kuongezwa ili kuwawezesha wanafunzi kusoma baada ya kuwa nyumbani kwa muda.